31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

MADEREVA BODABODA, DALADALA KUWALINDA WANAFUNZI WASICHANA

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


MADEREVA wa bodaboda na daladala wamepewa kazi ya kuwalinda wanafunzi wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao za kupata elimu bila kukumbana na vikwazo.

Kupitia kampeni iliyozinduliwa na Taasisi ya Wanawake Katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI), madereva wa bodaboda, makondakta na madereva wa daladala, watapata elimu ya kuwalinda wanafunzi wa kike kutumbukia katika masuala ya ngono kutokana na changamoto za usafiri.

Akizungumza katika maandamano yaliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Wajiki, Janeth Mawinda, alisema wameamua kupeleka elimu kwa kundi hilo kwa kuwa ndilo linalonyooshewa kidole katika kukwamisha maendeleo ya watoto wa kike.

“Tumeamua kupeleka elimu kwa kundi hilo kwa sababu ndilo linalonyooshewa kidole na jamii kuchangia kukwamisha masomo ya wanafunzi wa kike ambao wengi hupata mimba na kushindwa kuendelea na masomo.

“Wasichana wanashindwa kufikia malengo yao kutokana na kuwapo kwa rushwa ya ngono inayosababishwa na shida ya usafiri wanapokwenda shuleni.

“Tumeamua kupeleka kampeni kwa jamii hii ili watambue kuwa wana jukumu la kuwalinda watoto wanapokuwa njiani na wawaone kama wamewapakia watoto wao ama wadogo zao,” alisema Janeth.

Aidha mkurugenzi huyo aliongeza wameamua kuishirikisha jamii kuhakikisha inawalinda watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao na kufikia 50 kwa 50 katika uchumi wa viwanda.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai, alisema takwimu zinaonyesha asilimia 72 ya watoto wa kike wanakutana na ukatili wa kijinsia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles