25.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Pakistan yatoa msaada mapambano ya corona

Aveline Kitomary -Dar Es Salaam

SERIKALI ya Pakistan imetoa msaada  wa vifaa mbalimbali  vyenye zaidi ya thamani ya Sh milioni 11 ikiwa ni sehemu ya kuisaidia nchi kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Vifaa vilivyotolewa ni barakoa  za upasuaji 1,800, kofia ambazo zinavaliwa na  wahudumu wa afya wakati wanahudumia wagonjwa 1,800, kava za viatu za kuvaliwa wodini 800, barakoa za N95 zipatazo 500, magauni ya kuvaa watoa huduma za afya 100, glovu 8,000 pamoja na miwani 60 za kujikinga na virusi.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mwakilishi wa Ubalozi wa Pakistan hapa nchini, Muhammad Saleem, alisema kuwa wanaipongeza  Serikali kwa jitihada zinazofanyika katika kukabiliana virusi vya corona nchini.

Saleem alisema tangu ugonjwa huo ulipoingia  hapa nchini mwezi uliopita, kasi ya maambukizi ni ndogo ukilinganisha na nchi zingine, hiyo yote ni kutokana na hatua thabiti zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.

“Nchi yetu ya Pakistan imekuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania, hivyo basi  tumeona nasi tutoe msada wa vifaa kinga.

“Tunaomba mpokee mchango wetu ambao ni kidogo ili watoa huduma wa afya waweze kutumia vifaa hivi wakati wanawahudumia wagonjwa kwani ugonjwa huu ni janga la dunia,” alisema Saleem.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa  Muhamad  Kambi, aliushukuru ubalozi wa Pakistan kwa msaada walioutoa na kusema kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa Covid -19 ni janga la dunia,  watu wengi wamepata madhara kutokana ugonjwa huo, hivyo basi hakuna msaada mdogo, msaada wowote unaotolewa kwa Serikali utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na ugonjwa,” alisema Profesa Kambi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles