24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

OSHA yawataka wadau kutoa ushirikiano

Mwandishi wetu

WAKALA wa Usalama Mahala pa Kazi nchini (OSHA), imewataka wadau nchini kuendelea kutoa ushirikiano kwa ili kuboresha hali za wafanyakazi maeneo ya kazi.

Wito huo ulitolewa jana Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Usalama na Afya, Mhandishi Alex Ngata kwa niaba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Osha, kwenye mafunzo ya Vision zero yaliyoandaliwa na Osha, ambapo aliwataka wadau kuendelea kutoa ushirikiano ili kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi Maeneo ya kazi, kwa kuhakikisha kuwa usalama na afya sehemu za kazi vinazingatiwa.

Alisema Osha imeendelea kuboresha huduma zake kwa wadau hao, hivyo hawanabudi kuhakikisha wanashirikiana wakati wote kwa kuzingatia kuwa kaguzi zote za kisheria zinafanyika ili kukidhi matakwa ya sheria.

“Kama mnavyofahamu kwamba Osha inafanyakazi kwa karibu zaidi na wadau hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha kuwa mnaendelea kutoa ushirikiano ili kuboresha hali za wafanyakazi kwenye maeneo ya kazi.

“Kwani Osha imeboresha huduma zake kwa kuondoa tozo ambazo ni ada ya usajili sehemu za kazi, leseni ya kukidhi matakwa ya sheria, tozo ya vifaa vya kuzima moto, fomu ya usajili ambazo zilikuwa kikwazo kwa waajiri kwa kuziondoa na zingine na hivi karibuni tumepunguza tozo ya
uchunguzi wa ajali sehemu ya kazi ili kuwezesha waajiri kukidhi matakwa ya sheria,” alisema Ngata. 

Upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu wa Osha, Joshua Matiko alisema ili kuweza kufikia malengo hayo, waajiri nchini wanatakiwa kuweka mifumo madhubuti ya kulinda wafanyakazi wakiwa kazini, ikiwemo kuweka malengo kwenye mipango mikakati yao wanayopanga.

“Menejimenti ndio wenye jukumu la kusimamia masuala ya usalama sehemu za kazi kwani wasipoweka juhudi basi nivigumu kufanikiwa,” alisema Matiko.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za tathimini kutoka Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) Dk. Abdulasum Omary alisema watu takribani milioni 2.3 wanapoteza maisha sehemu za kazi kila mwaka kutokana na ajali na magojwa yanayotokana na kazi.

Wakizungumza mara baada ya mafunzo hayo baadhi ya washiriki waliishukuru Osha kwa mpango huo wa kuona umuhimu wa kuwapa mafunzo na kwamba yatawasaidia kuboresha utendaji wao.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles