24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ni hatari kunywa maji mengi iwapo tezi dume imeathirika

Aveline Kitomary

TEZI Dume (Prostate) ni ki-
ungo ambacho kinajihusisha na uzazi kwa wanaume ambapo kila mwanamume ili awe kamili lazima kuwa nayo.

Tezi hii zinahusika na mfumo wa uzazi ambapo mbegu za uzazi zinatengenezwa halafu husafirish- wa na kuhifadhiwa, wakati mwa- namume anapojamiiana mbegu zinapita kwenye tezi na kumwagika nje.

Tezi dume pia inakazi ya kuzali- sha vichocheo vinavyosafisha njia inayopitisha mbegu zinazotoka zisiwe na madhara kwa sababu njia hiyo pia hupitisha mkojo.

Pia vichocheo hivyo vinaongeza ujazo wa majimaji yale ambayo yanabeba mbegu za mwanamume kwahiyo hii tezi ni muhimu kwa mwanamume yoyote.

Wakati mwingine tezi dume in- aweza kupata madhara kama ilivyo viungo vingine vya mwili.

Zaidi ya theluthi ya wanaume wote walioko juu ya miaka 50 wa- nadalili za kuvimba kwa tezi dume.

Haijajulikana kwa uhakika ni kwanini tezi dume huwa kubwa zaidi kwa kadiri umri unavy- oongezeka lakini kukua huko
sio dalili ya saratani na wala hakuongezi uwezekano wa kupata saratani.

Wataalamu wa afya wanabaini- sha kuwa wanaume wasiofanya mazoezi wako hatarini kupata matatizo ya tezi dume.

Wengine waliko hatarini ni wa- naume wanaopenda kula vyakula yenye kiasi kikubwa cha mafuta kwani uwapo wa sumu nyingi na mafuta mengi mwilini hasa katika mishipa na ogani za uzazi huweza kuleta matatizo.

Na wengine huweza kuathirika baada ya matumizi ya pombe kali, uvutaji wa sigara, uzito mkubwa, kutokukaa sawa kwa vichocheo, umri mkubwa, historia ya familia, magonjwa ya zinaa na mengineyo.

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya wanaume 10, wanaume watano na kuendelea wanadalili za kuta- nuka kwa tezi dume.

Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo na Uzazi kwa Wanaume, ku- toka Hospitali ya Taifa ya Muhim- bili (MNH), Dk. David Mgaya, anasema tezi dume kama ilivyo viungo vingine vya mwili inaweza kupata madhara na kuumwa hivyo ni muhimu jamii kuzingatia hilo.

“Tezi dume inauhusiano na mkojo kwani mfumo wa mkojo huanzia kwenye figo kuelekea kwe- nye mirija hadi kwenye kibofu hadi kutoka nje hivyo ugonjwa wowote kwenye tezi huleta dalili kwenye mfumo wa mkojo.

TATIZO LINAVYOTOKEA

Dk. Mgaya anasema tezi dume ikiumwa inavimba na kuwa kubwa hali hiyo huweza kuziba njia ya mkojo baada ya kutanuka na kukar- ibiana na njia hiyo.

Mwanaume akipimwa tezi dume

“Kwa kawaida tezi ni ndogo gramu 15 lakini kadiri mwana- mume anavyokua kuna vichocheo vinavyozalishwa ambavyo vinaitwa ‘testosterone’ hii inasababisha tezi inakua kadri umri unavyoongezeka.

“Homoni hizi za ‘testosterone’ pia zinahusika kwenye ukuaji wa mfumo wa uzazi kwa mwanamume tangu akiwa tumboni via vya uzazi vya ndani na vya nje vinategemea homoni hizo.

“Huzalishwa kwa wingi kipindi mtoto akiwa tumboni hadi miezi mitatu, lakini baada ya hapo zina- pungua na baadaye kuja kuongeze- ka tena wakati wa balehe,” ana- fafanua Dk. Mgaya.

Anasema baada ya balehe homoni hizo hupungua mwilini kwa sababu wakati huo huwa kuna mabadiliko kadhaa.

“Mvulana anapo balehe homoni huanza kutumika mfano kufanya sauti kuwa nzito, ndevu na nywele sehemu mbalimbali za mwili zote zinategemea homoni hizo.

“Umri ukishasogea matumizi ya ‘testosterone’ katika sehemu nyingine za mwili zinapungua zaidi kwahiyo inatumika zaidi kwenye tezi dume, kadri homoni hizo zinavyoendelea kuongezeka na umri kuongezeka, misuli ya tezi inaongezeka na kuwa kubwa.

“Ikishakuwa kubwa inafinya au

kuziba njia ya mkojo ndio hapo sasa mtu anaanza kuwa na dalili kwenye mfumo wa mkojo.

“Lakini pia inawezekana sio kuwa kubwa tu, unaweza kupata saratani kama sehemu zingine
za mwili na ukipata saratani kwa sababu mfumo wa mkojo unapita utakuwa na dalili za mkojo na dalili katika mfumo wa uzazi pia,” ana- bainisha Dk. Mgaya.

Anasema hali hiyo ikitoka mkojo hushindwa kutoka nje au kutoka kidogo bila kumalizika.

“Ukiwa na mzigo wa mkojo, mfano mkojo kutokuisha kibofu kinaanza kuathirika na mkojo huwa na acid inayoitwa Uric Acid, ikit- uama kwenye kibofu mtu atapata maambukizi ambayo pia yanaweza kusababisha kutengeneza mawe kwenye mafumo wa mkojo.

“Lakini pia kama mkojo hautoki wote na kuisha, kibofu kinatanuka, kwa kawaida mwili wa binadamu uwezo wa kibofu kutunza mkojo ni mill 350 hadi 500 ikifika 450 hadi 500 lazima ukakojoe.

“Kama kuna mzibo mkojo uta- baki mwingi kwenye kibofu na mi- suli ya kibofu cha mkojo itaathirika baadae mirija inayoleta mkojo kutoka kwenye figo kupeleka chini itaathiri na figo zitaathirika na itashindwa kufanya kazi,” anaeleza.

Anasema endapo kama chumvi

chumvi ambazo zimezalishwa humo hazitatoka zitachukuliwa na kurudishwa kwenye mzunguko wa mwili kwa sababu mwili unatabia hiyo.

“Ile chumvi ikirudi kwenye mwili mgonjwa anaweza kuone- sha dalili za shida ya figo kama kichefuchefu, kutapika na men- gine,” anasema.

DALILI

Kwa mujibu wa Dk. Mgaya, dalili za mwanamume kuwa na tatizo kwenye figo ni pamoja na kutoku- maliza mkojo hivyo mkojo kubaki kwenye kibofu.

“Dalili zingine ni kuziba kwa njia ya mkojo, kwenda kukojoa mara kwa mara, kuamka usiku kukojo mara nyingi, kupata maam- bukizi katika njia ya mkojo na wakati mwingine kukojoa damu.

VITU HATARISHI

Dk. Mgaya anasema unywaji wa maji mengi usiku wakati tayari tezi dume imekuwa kubwa ni hatari kwa sababu mkojo unaozalishwa unakuwa mwingi na hauishi kuto- kana na kutokufanya kazi yoyote usiku.

“Ukinywa maji mengi jioni utapata mkojo wa mara kwa mara tofauti na mchana mgawanyiko wa maji ni mkubwa lakini mtu ana-

poenda kulala mkojo utachujwa na kuwa mwingi hivyo lazima utabaki zaidi kwenye kibofu,” anabainisha. Anasema unywaji wa pombe

pia unaweza kusababisha mkojo kuongezeka hivyo kufanya dalili ya tatizo la tezi dume kuongezeka zaidi.

“Unywaji wa kahawa wakati
wa jioni hufanya dalili kuonekana zaidi, kuna wengine wakiepuka kunywa kahawa, maji na pombe wakati wa jioni mtu anaweza kue- lekezwa akabaki kufuata taratibu na akaishi bila kufanyiwa upasuaji kama dalili zake hazikufikia hatua za kuziba mkojo lakini kwa wale ambao wameziba zaidi hawa wana- hitaji matibabu.

“Kuna watu ambao wanavinasa- ba ambavyo vinasababisha tezi zao zinakuwa kubwa zaidi hivyo tatizo hilo linakuwa ni la kurithi kwao hao utakuta watakuja na dalili chini ya umri wa miaka 55 kwa sababu sisi tunategemea miaka 55 kwenda juu,” anafafanua Dk. Mgaya.

TOFAUTI YA SARATANI NA TATIZO LA TEZI DUME

Kwa mujibu wa Dk. Mgaya, saratani ya tezi dume na tezi dume iliyovimba inatofautiana kutokana na dalili za saratani kuambatana na maumivu ya mgongo na kama haijatibiwa inaweza kusababisha

kupooza miguu, haja ndogo na kubwa kutoka bila taarifa na pia itasambaa sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo mapafu na ubongo.

“Kila mwanamume ana tezi dume lakini sio wanaume wote wanapata shida ya tezi dume, hii inategemea na vichocheo vina- vyokufanya dalili kuonekana na hakuna uhusiano kati ya saratani ya tezi dume na tatizo la tezi dume lakini huenda majeraha kwenye tezi dume yanaweza kusababisha saratani,” anaeleza.

VITU VYA KUZINGATIA KULINDA TEZI DUME

Kwa mujibu wa Dk. Mgaya, tati- zo la tezi dume hutibiwa kulingana na hatua iliyofikia hasa endapo mtu atawahi hospitalini.

“Kuna mwingine anapewa ushauri na anaendelea na maisha kama kawaida na kama yuko dalili za mwanzo mfano tayari mfumo wa mkojo umeziba anaweza ku- fanyiwa upasuaji,” anafafanua Dk. Mgaya.

Anashauri: “Kuacha kuvuta sigara, matumizi ya pombe kali, watu waache kukaa sehemu moja kwa muda mrefu na kufanya mazoezi, wanaume waache kuvaa nguo zilizobana wataepukana na maradhi mengi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles