Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wafanyakazi wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) wameungana na Wafanyakazi wengine nchini na duniani katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani Mei Mosi.
Maadhimisho ya mwaka kitaifa yanafanyika jijini Dodoma ambapo, mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani huku yakiongozwa na kauli mbiu ya Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ndiyo kilio chetu: kazi iendelee.
Watumishi wa OSHA wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda wameshiriki maadhimisho hayo kitaifa kwa maandamano pamoja na Wafanyakazi wengine yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma na kupokelewa na Rais Samia.
