31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Omog afuta makosa

Joseph Omog
Joseph Omog

* Kuivaa Azam kwa kujiamini

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BAADA ya kuona kikosi chake kimepoteza nafasi nyingi za kufunga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, kocha mkuu wa timu ya Simba, Joseph Omog, juzi alifanyia kazi mapungufu hayo katika mazoezi ya jioni yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veteran, Dar es Salaam, tayari kwa kuivaa Azam.

Omog ambaye anahitaji ushindi katika kila mechi, amekua pia akikataa ushindi mwembamba unaoweza kuwagharimu mbeleni na timu yake.

Akizungumza juzi baada ya mazoezi, Omog alisema alikua anafanyia kazi jinsi ya kutumia vema nafasi za mwisho zinazotengenezwa na viungo ambazo washambuliaji wake wanashindwa kuzimalizia.

“Kikosi kilikuwa na matatizo ya umaliziaji na ndio maana nimeona ni vema kuyafanyia kazi mapema kabla ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC, ambapo pia yatanisaidia kutafuta kikosi cha kwanza kitakachoanza.

“Katika mchezo wetu na Mtibwa licha ya kupambana na kushinda bao 2-0, wachezaji walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini walifeli kwenye umaliziaji.

“Tumerekebisha vya kutosha na tupo tayari kuivaa Azam huku tukiwa tunajiamini,” alisema.

Simba itacheza na Azam Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles