24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Waziri Mkuu yabaini udhaifu urejeshwaji mikopo ya vijana

Derick Milton, Simiyu

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu imebaini uwepo wa udhaifu kwenye halmashuari za Mkoa wa Simiyu katika kufuatilia urejeshwaji wa fedha zinazotoka mfuko wa maendeleo ya vijana.

Fedha hizo ambazo hutolewa na ofisi hiyo kwa ajili ya kuwakopesha vijana, zimekuwa hazirejeshwi kwa wakati kama inavyotakiwa kutokana na waliokopeshwa kutofuatiliwa kwa karibu.

Hayo yamesemwa leo Julai 5, na Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi hiyo Amosi Nyandwi, wakati akiongea na maafisa vijana, wakurugenzi na maafisa mipango wa mkoa huo Mjini Bariadi.

Nyandwi amesema halmashuari zote kwenye mkoa huo zimeshindwa kuwafuatilia kwa karibu vijana ambao walikopeshwa fedha hizo, hali ambayo imesababisha wengi kushindwa kuzirejesha.

“ Tumekuta kwenye fedha hizo na zile asilimia 10 za mapato ya ndani kuna utofauti mkubwa kwenye kurejeshwa, asilimia 10 zinarejeshwa kwa wakati na vijana wanafuatiliwa lakini hizi za kwetu hazifuatiliwi hatujui tatizo ni nini?” amehoji Nyandwi.

Kwa upande wao baadhi ya maafisa vijana kwenye halmashauri walilalamikia utaratibu wa mikopo ambayo hutolewa kwa vijana kutokuwepo na kifungu za kuwawezesha wao kufanya ufutiliaji na utoaji wa elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles