21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisi ya AG yaanza kupitia mapendekezo ya Sheria ya Huduma za Habari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), inapitia mapendekezo ya Sheria ya Huduma za Habari baada ya kukabidhiwa kutoka Ofisi ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Hatua hiyo inafanyika kabla ya Ofisi ya AG kuwasilishwa Muswada wa Mapendekezo ya Sheria ya Huduma za Habari bungeni ili kusomwa kwa mara ya kwanza, ya pili na hatimaye kupitishwa kuwa sheria.

Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano ya Habari, Nape Nnauye amethibitisha kwamba, maoni na mapendekezo ya wadau mpaka sasa yamekabidhiwa katika ofisi wa AG kwa kuwa utaratibu unaelekeza hivyo.

“Kuhusu mchakato wa mapitio ya sheria za habari Namba 12 ya Mwaka 2016, nafurahi kuwajulisha kuwa baada ya majadiliano ya muda mrefu na wadau mbalimbali, hatimaye majadilioano yamekamilika na nyaraka za maeneo yote tuliyokubaliana kufanyia mabadiliko zimewasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu,” amesema Nape akiwa jijini Dodoma wakati akizungumzia hatua zilizofikiwa kuhusu mchakato mabadiliko sheria ya habari.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile amesema mchakato huo mpaka kufikishwa bungeni una hatua zake na kwamba, inachofanya serikali ni utaratibu wa kawaida wa kazi katika kuelekea mabadiliko ya sheria hiyo.

“Mchakato bado upo kwenye mstari ule ule, mpaka sasa matumaini yetu yapo juu katika kufikia kile tunachokihitaji. Serikali bado inapitisha mapendekezo yetu katika hatua zile zile za kawaida.

“Sisi tungetamani kasi zaidi kama alivyoshauri Mheshimiwa Rais Samia (Sukuhu Hassan) kwamba, tulimalize,” amesema Balile akizungumzia kauli ya Nape kwamba, mapendekezo ya wadau wa habari yapo katika ofisi ya AG.

Muungano wa wadau wa habari (CoRI) umefanya vikao viwili na serikali katika kuelekea mabadiliko ya sheria ya habari.

Wadau hao nchini wanashauri marekebisho kwenye vipengele mbalimbali vya sheria hiyo ikiwa ni pamoja na kifungu cha sita (e) kinachoeleza magazeti kupatiwa leseni kila mwaka badala ya usajili wa moja kwa moja.

Pia marekebisho dhidi ya kifungu cha saba (2) (b) (iv) kinachoelekeza vyombo vya habari kutangaza au kuchapisha habari na masuala yenye umuhimu kwa Taifa kadiri itakavyoelekezwa na serikali, wadau wakielezea kuwa kipengele hiki kinaingilia uhuru wa uhariri.

Sheria nyingine zinazolalamikiwa ni pamoja na ile ya mawasiliano ya kielektroniki na huduma za posta (EPOCA, 2010), sheria ya Makosa ya Mtandao (2015), sheria ya Haki ya kupata Habari (2016) na kanuni za Maudhui Mtandaoni (2018).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles