30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Nyota Stars wanaokipiga Simba, Yanga kufuatiliwa

Na WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, anatarajia kutumia mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga , kufuatilia viwango vya wachezaji ambao amekuwa akiwajumuisha katika kikosi chake.

Ndayiragije atakiongoza kikosi cha Taifa Stars  kitakachoshiriki fainali za Mataifa Afrika kwa   Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (Chan), ambazo zinatarajia kutimua vumbi kuanzia Aprili 4 hadi 25 nchini Cameroon.

Akizingumza na MTANZANIA, Ndayiragije, alisema atakuwepo kwenye dimba la Taifa, kufuatilia mchezo huo kama alivyofanya katika mechi nyingine.

Alisema anajua ana kazi ngumu ya kutengeneza kikosi imara, licha ya kwamba maandalizi yameanza muda mrefu baada ya kufuzu michuano hiyo.

“Hakuna mechi nakosa kuingalia kwa sababu ni jukumu langu kama kocha wa timu ya Taifa, wachezaji wangu wapo katika timu zote Tanzania, ni lazima nifuatilie maendeleo yao,” alisema Ndayiragije.

Stars imepandwa Kundi D katika michuano hiyo na itazindua kampeni zake Aprili 7 kwa kuumana na Zambia.

Nchi nyingine zinazounda kundi hilo ni Namibia na Guinea.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles