27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Kotei akumbuka mchezo wa watani

Na WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

KIUNGO wa zamani wa Simba, James Kotei, bado hajaisahau raha ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, baada ya kusema leo ataketi mahali tulivu kuufatilia ‘live’.

Timu hizo zitaumana, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kuanzia saa 11 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kotei aliicheza Simba kwa mafanikio makubwa, akiisaidia kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, kabla ya kutimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kisha FC Slavia-Mozyr ya Belarus.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kotei alisema mchezo huo ni mkubwa hivyo ataungana na Wanasimba kuisapoti timu yake hiyo ya zamani.

“Najua kama kesho ni mchezo wa ‘derby’ ya Kariakoo, nitaangalia mechi hii hapa hapa nilipo, nakumbuka shamrashamra zake, Simba Nguvu Moja.

“Kitu kikubwa ninachokumbuka katika mchezo huu ni jinsi mashabiki wanavyoufanya mchezo huo kuwa na mvuto wa aina yake na ndicho kinanifanya niangalie,”alisema Kotei.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles