Nyemo SOA atoa siri ya ‘Jaka Roho’

0
1391

Christopher Msekena

MKALI wa Bongo Fleva, Nyemo Roby a.k.a Nyemo SOA, amesema mapokezi mazuri na ngoma yake mpya, Jaka Roho ni matunda ya maandalizi aliyoyafanya kwa muda mrefu.

Akizungumza na MTANZANIA jana,  Nyemo alisema alikaa kimya kutoka mwaka 2014 ili kujipanga na kufanya kazi zitakazokonga nyoyo za mashabiki zake.

“Nashukuru Jaka Roho inafanya vizuri kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii na runinga mbalimbali, naamini mashabiki zangu walikuwa wananisubiri kwa hamu, nimerudi kivingine hivyo watarajie ngoma juu ya ngoma, video ya Jaka Roho tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema Nyemo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here