22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

NONDO KUANDAA WARAKA KUELEZEA YALIYOMKUTA

Na Asha Bani, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo amesema anaandaa waraka kuelezea yaliyomkuta hadi kupata dhamana.

Aidha, amesema hana taarifa za kusimamishwa kwake na chuo kwa kuwa hajapewa barua yoyote hadi sasa.

“Napumzika kwanza afya yangu si nzuri kiakili, siko vizuri najiandaa kuelezea yaliyonisibu ndani ya siku hizi mbili nitawatafuta wanahabari kuwaeleza.

“Sina mawasiliano ya simu hata moja sijui chochote nachungulia kwenye simu za wenzangu ndiyo naona kwamba nimesimamishwa chuo,” amesema Nondo.

Nondo amesema hayo leo Jumanne Machi 27, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kupata dhamana jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.

Pamoja na mambo mengine, amesema anawashukuru Watanzania kwa kupaza sauti hasa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Askari wa Magereza Iringa ambao amekaa nao vizuri.

Kwa upande wake Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema wanakwenda makahamani kupinga Nondo kusimamishwa na kuondolewa kwa vifungu ambacho vyuo wanatumia kuwasimamisha kwani havina mantiki kwa katiba ya nchi.

“Hata Mahakama ya Iringa imesema wampe dhamana akaendelee na masomo na hata kwenye taasisi nyingine ndiyo inavyokuwa hivyo.

“Kwa mfano akikamatwa mfanyakazi wa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) mtasema apishe uchunguzi lakini si shule, kwanza hawakuwa wanafanya kazi zao kwenye chuo ni nje ya chuo haihusiani na kuwasimamisha kabisa,” amesema Olengurumwa.

Nondo yuko nje kwa dhamana akishtakiwa kwa makosa makosa mawili, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kuwa alitekwa ambapo mahakama imempatia dhamana na wakati huo huo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kimemsimamisha chuo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles