23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yafunga Mfumo wa Oxygen Hospitali ya Chanika

Na Mwandishi Wetu, Dae es Salaam

Benki ya NMB kupitia kwa wafanyakazi wake Idara ya Treasury, imekabidhi kiasi cha Sh milioni 3.8 kwa uongonzi wa Hospitali ya Chanika iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam, ili kuwezesha ufungaji wa Mfumo wa Oxygen katika hospitali hiyo.

Kiasi hicho cha pesa kimechangwa na wafanyakazi hao na kukabidhiwa leo, ambapo ufungwaji wa mfumo wa Oxygen katika Hopsitali hiyo, utaokoa maisha ya mama na watoto ambao wamekuwa na uhitaji mkubwa.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB Idara ya Hazina wakiongozwa na Meneja Mwandamizi Idara ya Hazina, Samira Saleh (wa tatu kulia) wakikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu na laki nane na sabini na tano (3,875,000/-) kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chanika, Barnabas Mtumbuka (mwenye fulana ya mistari katikati) zilizotolewa na wafanyakazi wa idara hiyo ili zitumike kugharamia mfumo wa Oxygen kwa wagonjwa Hospitali ya Chanika jijini Dar es Salaam.  Wengine ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Chanika Ally Mzaha (wa pili kushoto) pamoja na Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Scolastica Rimoy (kushoto).

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Mwakilishi wa Idara ya Treasury NMB, Samira Saleh aliishukuru Ofisi ya Mganga Mkuu kwa ushirikiano uliofanikisha makabidhiano hayo na kwamba wanaamini msaada huo unaenda kuokoa maisha ya mama na mtoto wanaohudumiwa hospitalini hapo.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza vifo vya mama na mtoto, Kama alivyotuasa Rais Samia Suluhu Hassan kuchangia harakati za kuwavusha salama mama na mtoto, tumeamua kuchangia kiasi hiki ili kufunga Mfumo wa Oxygen hapa, ili kusaidia takribani kina mama 30 wanaojifungulia hapa kila siku.

“Tunaamini msaada huu unaenda kujenga mazingira salama ya kimatibabu kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU), Neonatal Care Unit (NCU) na Emergency Unit, hivyo kupunguza uhitaji wa rufaa kwenda Hospitali za rufaa Amana na ya Taifa Muhimbili,” alisema Samira.

Awali akizungumza Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Willy Sangu, alisema Hospitali ya Chanika imekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa hapo, hasa kutokana na ongezeko la watu na makazi eneo la Chanika, na kwamba Mfumo wa Oxygen unaofungwa kwa msaada huo, utawasaidia wengi katika wodi mbalimbali, hasa kwenye kipindi hiki cha uwepo wa changamoto za upumuaji.

Wakati huo huo benki hiyo imetoa msaada wa meza 60 na viti 60 kwa Shule za Msingi Mtambani na Mgeule, zilizopo Tabata, Ilala jijini Dar es Salaam, vyenye thamani ya Sh. Milioni 14, huku ikitoa mabati 170 yenye thamani ya Sh. Milioni 5 kwa ajili ya shule shikizi Mnauka iliyoko Wilani Newala Mkoani Mtwara.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa Meza na viti, Meneja wa benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alisema meza na viti hivyo vyenye thamani ya Sh. Mil. 14, ni sehemu ya mpango wao wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), inayoendeshwa kwa miaka kadhaa sasa kupitia asilimia moja faida ya NMB kila mwaka, inayotumika kusaidia sekta za elimu, afya na majanga.

“Tunatoa meza 30 na viti 30 kwa kila shule, tukiamini msaada huu sasa unaenda kuboresha mazingira ya kufundishia kwa kuwaongezea ari ya utekelezaji wa majukumu yao waalimu wa Mtambani na Mgeule kwa ustawi wa elimu ya watoto wanaosoma hapa,” alisema Richard.

Kwa upande wake, DC Ludigija alikiri kuwa Sera ya Elimu Bure imeongeza idadi ya wanafunzi mashuleni, hivyo kusababisha changamoto nazo kuwa nyingi na kwamba Serikali inajivunia na kuhitaji uungwaji mkono kutoka kwa wadau wa sekta hiyo Kama ambavyo NMB imejipambanua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles