28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kuendelea kuwalinda wawekezaji wa ndani

Na Safina Sarwatt, Rombo

Serikali Mkoani Kilimanjaro, imesema itaendelea kuwalinda wawekezaji wa ndani ambao wameonesha nia ya kuwekeza kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa jamii.

Kauli hiyo umetolewa Mei 2,2021 Wilayani Rombo na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Mshikizi Onesmo Buswelu, wakati alipotembelea banda la kiwanda cha kuzalisha Maji na Juisi cha Bella View Kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi ambazo kimkoa zilifanyika Wilaya ya Rombo na kuelezwa mchango wa kiwanda hicho kwa wakazi wa wilayani humo, kupitia sekta ya kilimo na ajira.

Buswelu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Siha, amepongeza juhudi zilizofanywa na uongozi wa kiwanda hicho katika sekta hiyo na kusisitiza kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Ilani yake
ya uchaguzi 2020/2025 kitaendelea kuthamini na kusimamia haki za wawekezaji wa ndani.

Awali akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi, Meneja wa Utawala wa kiwanda cha kuzalisha Maji na Juisi Bella View Fresh Fruit Processing Industry, Noah Ombeni, amesema kiwanda hicho kinazalisha Maji na bidhaa nyingine ikiwemo Juice ya Maembe, Ukwaju na Rozela.

Akizungumzia suala la masoko Ombeni amesema wanazo Kanda Nne ambazo wanauza maji hayo, ikiwemo Kanda ya Pwani, Kanda ya ziwa, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati.

Aidha, Ombeni ameiomba Serikali kuipitia upya sheria ya ulipaji kodi za maji kwani zimekuwa kandamizi jambo ambalo limekuwa likiwaumiza wawekezaji.

“Tunaiomba Serikali itupunfuzie gharama ya kodi katika upande wa maji, kwani kwa sasa kodi ambayo tunatozwa kwa upande wa maji ni Shilingi 58 kwa lita, Serikali inatakiwa kutambua kwamba bidhaa ya maji ni kwa ajili ya afya ya binadamu na sio kwa ajili ya biashara,”amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Maabara Joseph Rabaga, amesema wakati wa kiangazi mito mingi hukauka kutokana na vyanzo vya maji kukauka na hivyo kusabaisha uzalishaji wa bidhaa hizo kupungua.

“Kiwanda cha Bella View Fresh Fruit Processing Industry huzalisha katoni milioni moja kwa mwaka, lakini wakati wa kiangazi bidhaa hizo hupungua kutokana na vyanzo vya maji wanayoyategemea kukauka,”amesema Rabaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles