27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Njia rahisi kuacha tabia usiyoipenda

Ha CHRISTIAN BWAYA

UENDA umewahi kuteseka ukitafuta kujua namna unavyoweza kuachana na tabia usiyoipenda. Nazungumzia zile tabia zinazokufanya ujione mtumwa unayebeba mzigo usiobebeka.

Mtumwa unayejua unataka kuachana na uzinzi lakini huwezi. Hupendi kutumia simu unapokuwa katikati ya mazun- gumzo na watu lakini huwezi kuacha.

Unatamani kuacha uongo lakini unashindwa. Unaishi na uraibu na unajiona huna namna ya kujinasua. Unajiuliza tatizo ni nini?

Wapo wanaoamini kuwa kuna watu wanashindwa kuacha tabia zinazowatesa kwa sababu hawajui madhara yake.

Mtazamo huu una matatizo kwa sababu wakati mwingine unajua madhara lakini bado unafanya yale yale unayoyajua. Unajua uzinzi holela unahatarisha maisha yako kwa magonjwa ya zinaa lakini bado hauachi.

Unajua fika kuwa sigara inaweza kukusababishia saratani ya mapafu lakini bado unavuta. Kwanini hauwezi kuacha tabia unayofahamu madhara yake?

Ukweli ni kwamba, kujua hai- toshi. Uelewa wa mambo na tabia ni vitu viwili tofauti. Unaweza kujua jambo kwa upana wake lakini ukaishi tofauti kabisa na yale unayoyajua. Wakati mwingine wanaojua matokeo ya uhalifu ndio wanaoongoza kuufanya.

Hiyo ina maana kuwa ipo nguvu nyingine inayohitajika kukufanya utende kile unachokijua.

Wengine wanasema ili uachane na tabia usiyoipenda, lazima ukae mbali na mazingira yanayokuhamasisha kutenda kile usichokipenda. Ikiwa, kwa mfano, unapambana kuachana na ulevi, jenga mazingira ya kukaa mbali na walevi na vilevi.

Ikiwa una tatizo la kujichua, basi epuka kukaa mwenyewe mwe- nyewe chumbani. Ingawa njia hii ya kubadili mazingira inaweza kukusaidia kuachana na baadhi ya tabia, wakati mwingine matokeo yanakuwa ya muda tu. Unaacha pombe kwa siku kadhaa, lakini inapotokea unakutana na mazingira ya pombe unarudi kule kule ulikotoka. Maana yake kujitenga

na mazingira yanayohamasisha tabia unayopambana kuachana nayo hakutoshi.

Ningependa katika makala haya nikusaidie kujifunza mbinu ya kuachana na tabia usiyoipenda. Ingawa mbinu hutegemea na aina ya tabia inayohusika, bado kuna mambo ya msingi yanayojenga uraibu ambayo ni muhimu kuyatazama.

Kwanza, ni ukweli kuwa uraibu unapaliliwa na ile raha inayotokana na tabia husika. Huwezi kuwa mtumwa wa tabia isiyokufanya ukajisikia vizuri hata kama huipendi. Ile raha inayoambatana na tabia inayokusumbua ndiyo hasa inayoufanya ufahamu wako ufanye juhudi za kuhakiki- sha huachi. Raha inakuwa kifungo chako.

Lakini pili, uraibu unaku- wa tabu kuuacha kwa sababu pamoja na kuwa mtu anakuwa haupendi hufika mahali ukawa sehemu ya utambulisho wake. Mwanzoni mtu huanza na jitihada za kujinanua na tabia anayojua
si nzuri.

Fahamu zake zinaamini anafanya kitu kisicho sahihi. Lakini bahati mbaya ile raha inayotokana na kufanya kisicho sahihi inakuwa sehemu ya maisha yake. Mtu huyu anajikuta amekuwa tegemezi na hawezi tena kuachana nayo kwa sababu tayari

anaanza kuamini maisha yake hayawezi kuwa na amani bila kufanya kile anachojua si sahihi.

Taratibu anaanza kuiaminisha akili yake kuwa hana anachoweza kukifanya tena. Kama ni tamaa za mwili, mtu huyu huanza kujiaminisha kuwa tamaa za mwili ni sehemu ya maisha yake. Anaanza kujiaminisha kuwa kile kibaya anachokifanya lakini kinachoambatana na raha fulani, hakina ubaya wa kiasi kile.

Fahamu zake zinaanza kupata faraja kuwa ana- chokifanya kinaweza kuwa sahihi kwa upande mwingine. Inapofikia hapo, inakuwa vigumu mtu huyu kujinasua na kongwa la uraibu.

Mabadaliko yanaanza kwa kubadili kwanza mtazamo. Unahitaji kuanza kukataa tabia uliyoanza kuikubali. Kataa kujifariji kuwa hicho unachokifanya ni sahihi hata kama wapo wengi wanaofanya kama wewe. Ulazimishe ufahamu wako uamini kwa dhati kuwa inawezekana kubadi- lika hata kama umejaribu mara kadhaa bila mafanikio. Hatua hii ni ngumu lakini muhimu.

Ikiwa umeanza kuamini hau- wezi kuishi bila simu, kwa mfano, huwezi kuzungumza na mtu bila kushika shika simu, huu ni wakati wa kukataa mazoea haya hata kama umeanza kuyachukulia kuwa sehemu ya maisha yako.

Ikiwa umeanza kuamini kutazama picha za ngono ni jambo la kawaida, anza kuiaminisha akili yako kuwa unachokifanya si sahihi hata kama umejaribu mara kadhaa kuacha lakini hujaweza.

Baada ya hatua hiyo ya kubadili kile unachokiamini, chukua hatua ya pili ya kujiaibi- sha. Ndio. Hauwezi kubadilika kwa kuendelea kulinda heshima yako. Unahitaji kujitengenezea maumivu ya kutosha kujisikia vibaya kuendelea kufanya kitu usichopenda kukifanya.

Kuna namna nyingi za kujiaibisha. Kwanza kabisa ni kumtafuta mtu anayekuheshimu na kumtobolea siri yako kuwa umekuwa na tabia usiyoipenda. Unapofanya hivi kwa vyovyote vile utahisi kujidhalilisha. Heshima yako itapungua lakini maumivu hayo ya kujidhalilisha yanaweza kuwa mwanzo wa uamuzi mgumu wa kubadilika.

ITAENDELEA
Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Mawasiliano 0754870815, twitter: @bwaya

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles