27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

Nini kipo jikoni mwa Tecno? 

Mambo vipi Tanzania? Katika pita pita zetu mtandaoni tumekutana na baadhi ya story za kunyapia nyapia  zinavyoashiria kuwa Tecno wapo jikoni. Kwa siku mbili sasa, kumekuwa na ‘countdown’ flan inayoendelea kimya kimya kwenye kurasa za mitandao ya kijami za kampuni nguli ya simu za mkononi nchini ya Tecno. Je kunani? Wanakuja na kitu kipya ama vipi? Tukaona isiwe mbaya, hebu tujaribu kuchunguza kidogo kujua nini kinaendelea?


Kutokana na aina ya matangazo yanayoonekana kwenye kurasa hizo, kuna uwezekano mkubwa wanazindua simu au kifaa kwenye ‘series’ yao mashughuri ya Camon. Camon ni series ya simu za Tecno ambazo ni maalumu kwa kufotoa mapicha picha, maselfie ya kibabe ya kuonyesha ulimbwende halisia. 

Pengine umekwisha zisikia C5, C8 na C9, swali linakuja tutegemee C nini? Ni C series au L series, ni compyuta au wamekuna na surprise kubwa zaidi? Hatuwezi kujua ambacho kimetokea, hata hivyo tunaweza kuzungumzia walau ambacho kimeshapita. 

Kutokana na maelezo hapo juu, nimeona si mbaya kama tutazizungumzia hizi C series japo kwa ufupi, ili kama wanakuja na C nyingine walau ujue zimetoka wapi, zilikuaje na sifa zake zilikuwa zipi? Kama vipi funga mkanda twen’ zetu. 

Tukianza na C5, ambayo ni kongwe zaidi kwenye series hii, ilikuwa na Camera ya nyuma yenye 8 MP ikipiga picha na kurekodi HD Video. Camera ya mbele ilikuwa na 2 MP pamoja na flash kwa mbele. 

Baada ya hapo ilifuata C8, hii waliiongezea nguvu zaidi kwenye upande wa Camera kwani ilikuwa nna Camera ya nyuma yenye 13MP na ile ya mbele Camera yake iliongezeka hadi 5 MP ikiwa na flash yake. Baada ya hapo ikaja baba leo, C9 ambayo yenyewe ina Camera ya Nyuma na Mbele zenye 13MP flash, maalumu kupiga selfie za kibabe, ushindwe wewe tu. 

Kama mawazo yetu juu ya Tecno kuja na series nyingine ya C unadhani itaitwaje? Na camera zake zitakuwa na sifa gani? Tuandikie kwenye comments mawazo yako. Pia tembelea tovuti hii kuanzia wiki ijayo, tutakuja kueleza hapa ni nini kimeletwa na Tecno. 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles