23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NEW ZEALAND KUPIGA MARUFUKU SILAHA ZA KIJESHI KWA RAIA

Christchurch, New Zealand

New Zealand itapiga marufuku silaha za aina yoyote zenye muundo wa kijeshi zilizotumika katika shambulio la mji wa Christchurch, Waziri Mkuu Jacinda Ardern amesema.

Sheria za matumizi ya bunduki nchini humo zimeangaliwa upya tangu mshambuliaji mwenye silaha kali alipowaua watu 50 katika misikiti miwili Ijumaa iliyopita.

Ardern ameeleza kwamba sheria ya kuruhusu marufuku hiyo itaidhinishwa wakati bunge nchini litakapokaa katika wiki ya kwanza ya Aprili na kuongeza kuwa anatarajia sheria hiyo mpya kuidhinishwa ifikapo Aprili 11.

Amesema watu wanaomiliki silaha hizo watasamehewa watakapozisalimisha na pia kutaidhinishwa mpango wa kuzinunua kutoka kwa wamiliki hao, kuruhusu kusalimishwa kwa silaha hizo.

Ardern aliongeza kuwa maafisa wanakadiria kwamba gharama ya kuzinunua upya silaha hizo kutoka kwa wamiliki huenda ikawa ni kati dola za marekani milioni 100 na 200 na kuwa hiyo ndio gharama ambayo ni lazima wailipe kuhakikisha usalama wa jamii yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles