23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NEC yasema haitaongeza muda wa uhakika tena

Na Safina Sarwatt-Kilimanjaro

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haitaongeza siku ya uhakiki wa daftari la kudumu la wapigakura, hivyo imewataka wananchi kutumia muda wa siku nne uliowekwa kisheria kufanya uhakiki wa taarifa zao mapema kabla kusitishwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi mkoani Kilimanjaro jana, ofisa wa tume hiyo, Zawadi Msala alisema  tume sasa iko kwenye hatua ya uwekaji wazi daftari la kudumu la wapigakura. 

Alisema uwekaji wazi daftari la wapigakura unafanyika nchi nzima kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa udiwani, ubunge na urais.

Msala alisema wapigakura wanatakiwa kutumia muda uliowekwa wa siku nne kwenda kufanya uhakiki wa taarifa zao na  tume haitaongeza muda tena. 

Alisema  uwekaji wazi utafanyika kuanzia  Juni 17 hadi 20. 

Msala alisema uhakiki huo utawahusu wapigakura wote nchi nzima waliojiandikisha kuanzia mwaka 2015 ambao bado hawajahakiki taarifa zao.

Jane Changamike kutoka NEC, alisema sasa  watu wanaohama wilaya kata limeshafungwa tayari, wale ambao taarifa zao zimekosewa watatakiwa kufika katika ofisi za halmashauri kurekebisha.

Alisema tume pia inawaondoa wale  ambao wamefariki dunia ambao majina yao yapo kwenye daftari la kudumu la wapigakura mara baada tu ya ndugu zao kutoa taarifa za kifo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles