25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mpango: Serikali itaendelea kufuatilia viashiri vya uchumi

Na Mwandishi Wetu -DODOMA

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema Serikali itaendelea  kufuatilia  mwenendo  wa viashiria vya uchumi na utekelezaji wa bajeti kwa ujumla na kama itabainika kutakuwa na haja ya kufanya marekebisho itafanya hivyo  wakati wa mapitio ya nusu mwaka Desemba.

Akihitimisha  kujibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2020-2021, Dk. Mapango alisema Serikali  itaendelea  kufuatilia  mwenendo  wa viashiria vya uchumi na utekelezaji wa bajeti kwa ujumla.

 “Na  kama itabainika kutakuwa na haja ya kufanya marekebisho ya bajeti, itafanya hivyo  wakati wa mapitio ya nusu mwaka  Desemba,” alisema Dk. Mapango.

Alisema Serikali imefuta tozo zaidi ya  60 ili kuhakikisha  wananchi wanakuwa na fedha za kuweza kujikimu wao na familia zao.

 “Na mnaona kabisa kwamba tumefanya uamuzi mkubwa wa makusudi, kwamba mwaka ujao wa fedha Julai mosi hatuongezi kabisa ushuru wa bidhaa, tumeshusha kiwango cha ‘skill development levy’, tumefuta tozo takribani 60 na yote tunafanya katika  kuhakikisha mfukoni wananchi wetu wanakuwa na fedha zaidi za kujikimu wao na familia  zao katika kipindi hiki kigumu,” alisema Dk. Mapango.

Alisema kupitia kaguzi mbalimbali, wamegundua kwamba mamlaka za hifadhi za taifa kuna upungufu mkubwa ambapo Serikali itatatua kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi.

Dk. Mapango alisema Hazina, Wizara ya Maliasili na Utalii na mamlaka za hifadhi  zitakaa pamoja kuandaa taratibu za kuhakikisha shughuli nyeti za uhifadhi ikiwa ni pamoja za  operesheni za dharura kukabiliana na ujangili.   

 “Tutafanya  hivyo kama ambavyo tunafanya pia kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na usalama vingine vyote ambavyo posho zao zinalindwa, na utaratibu  huu sio mpya ndio unaotumika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), pia unatumika mamlaka za viwanja vya ndege na inatumika kwa ufanisi,” alisema Dk. Mapango.

Kuhusu ugonjwa wa corona, alisema hakuna athari zozote kwenye uchumi zilizojitokeza na kwamba chakula kipo cha kutosha. 

 “Kwenye hotuba ya bajeti nilieleza  walifanya tathmini ya kiuchumi kati ya Januari na Aprili mwaka huu,  ilionyesha kwamba nchi yetu haijaathiriwa sana na ugonjwa wa corona ikilinganishwa na mataifa mengine.

 “Mauzo ya dhahabu yaliongezeka kutoka takribani Sh bilioni 743.8 hadi trilioni 1.5 ukilinganisha na mwaka  2019/2020,” alisema Dk. Mapango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles