27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

NAPE AITAKA SERIKALI KUJIPANGA UPYA BAJETI YA KILIMO

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), ameishauri serikali kuiondoa bungeni Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ili ikajipange upya na kuiboresha bajeti hiyo.

Pia amesema bajeti hiyo haina uhusiano wowote na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nape amesema hayo bungeni leo Mei 16, jijini Dodoma,  alipokuwa akichangia bajeti ya wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19 iliyowasilishwa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.

“Tatizo kubwa linaloikabili serikali ni kuwekeza fedha nyingi katika miradi mikubwa inayoweza kujiendesha yenyewe badala ya kuwekeza katika maeneo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi,” amesema Nape.

Hata hivyo, Nape alihoji mahali zinakopelekwa fedha wakati serikali inabana matumizi na kukusanya fedha nyingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles