22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

NANE NANE KITAIFA KUFANYIKA MIAKA MITATU MFULULIZO SIMIYU

|Mwandishi Wetu, SimiyuMaadhimisho ya Maonyesho ya Wakulima Nane Nane yatafanyika kitaifa mkoani somiyu kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020.

Hayo yamesema na Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba jana katika maonyesho hayo na kuongeza kuwa hatua hiyo ni kuongeza tija ya elimu katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa Mashariki.

Amesema kumekuwa na utaratibu wa kufanyika mfululizo maonesho hayo kwenye mikoa inayoandaa huku akieleza kuwa utashi uliopo katika kanda hiyo ni mkubwa ukilinganisha na maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika kwa miaka minne mfululizo katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

“Kufanyika mfululizo kwa miaka mitatu mkoani Simiyu kutawafanya wananchi kuwa na uhakika wa bidhaa za uwekezaji watakazoziweka.

“Mkoa wa Simiyu na kanda yenu hii ya magharibi ingetosha kuonyesha hata kwa miaka miwili tu lakini nimeamua kutumia utaratibu mzuri zaidi ili ifanyike kwa miaka mitatu naamini hamtaniangusha,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles