Namungo,Polisi Tanzania itafahamika leo

0
445

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

TIMU za Polisi Tanzania na Namungo FC, leo zitashuka dimbani kuonyeshana ubabe, katika mchezo wa  Ligi Kuu Tanzania, utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa, ulioko Ruangwa, Lindi.

Timu hizo zitakutana huku Namungo ikitoka kupata suluhu dhidi ya Kagera Sugar, wakati Polisi ilipoteza bao 1-0 na Azam.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti makocha wa timu hizo, kila mmoja alisema amesema anahitaji alama tatu.

“Hii ni mechi muhimu sana ukizingatia mchezo wa kwanza tulipoteza mbele ya Azam, tunahitaji ushindi ili kufuta machumng ya mechi ya kwanza,”alisema Malale Hamsini kocha wa Polisi Tanzania.

Kwa upande wake, Kocha wa Namungo, Hitimana Thiery alisema: “Tumeanza kwa sare ya bila kufungana, kwangu sio matokeo ninayohitaji msimu huu katika kusaka kutimiza malengo tuliyojiweka, tunatakiwa kushinda mchezo wa kesho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here