22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

NAIBU WAZIRI AAGIZA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA BAHI KUKUTANA


|Mwandishi Wetu, DodomaNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Bahi, mkoani Dodoma ikutane na kupanga mkakati wa namna bora ya kukabiliana
na ukataji ovyo wa misitu na kulinda mazingira.

Amesema ni lazima hatua za haraka zichukuliwe mara moja ikiwa ni pamoja na kuandaa taarifa ya ili ifanyiwe kazi nakuongeza kuwa suala la ulinzi wa misitu na mazingira halina mjadala.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua na kujionea hali ya uharibifu wa mazingira  wilayani Bahi, pamoja na mambo mengine  alishtushwa na kukithiri kwa wimbi la ukataji misitu ovyo wilayani humo kuagiza hatua za makusudi kuchukuliwa.

“Serikali wakati ikielekeza nguvu zake katika ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, suala la mazingira linapewa kipaumbele pia,” amesema Sima.

Sima pia amewataka viongozi wilayani Bahi kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazotekelezwa na serikali ikiwamo kulinda na kutunza mazingira kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadaye.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Rachel Chuwa amesema alisema halmashauri imekuwa ikishindwa kuwachukulia hatua wafanyabiashara kutokana na kuwa na vibali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Kuna wakati tunashindwa kuwachukulia hatua wafanyabiashara hao lakini pia hali hiyo imesababisha wafanyabiashara hao kuvitumia vibali hivyo tofauti na malengo kusudiwa ambapo mara kadhaa wamekuwa wakivitumia kuvuna badala ya kusafirishia mazao,” amesema.

Naye Meneja wa Kanda Wakala wa Huduma za Misitu (TSF), Mathew Kiondo ametolea ufafanuzi suala hilo na kukanusha kuwa ofisi ya Wakala Kanda  hawakuwahi kutoa vibali vya aina hiyo.

“Wakala kanda hatuhusiki na utoaji wa vibali vya aina hiyo, tumejipanga na kuelekeza nguvu zetu kupambana na waharibifu wa misitu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles