21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

MWANZA WAFURAHIA HUDUMA YA KUTUMA FEDHA BILA MAKATO

Mwandishi Wetu, Mwanza 

Siku chache baada ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, kuzindua huduma ya kutuma fedha bila makato, baadhi ya wananchi wa Jijini Mwanza wamefurahia wakidai Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati utafikiwa iwapo jamii itatumia mtandao huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara na mawakala wa Airtel Money, wamesema nchi nyingi zilizopiga hatua msingi wake umejengwa na mawasiliano ya uhakika ya kutuma na kupokea fedha bila makato.

“Zamani kabla ya huduma hii haijazinduliwa nilikuwa natuma fedha kwa Airtel Money lakini makato yalikuwa yanapunguza uwezekano wa kutuma fedha nyingi, lakini sasa ni kama vile nabadilisha fedha mkononi kwa kuwa hakuna makato tena,” amesema Mariam Othman mfanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Mwaloni.

Kwa upande wake Wakala wa Airtel, Faith Zebonius, amesema  tangu ilipoanzishwa  huduma  ya kutuma fedha  bila makato kumekuwa  na ongezeko la wateja wanaoomba kuunganishwa na mtandao huo hata huduma ya kutuma na kupokea fedha imeongezeka tofauti na awali.

Meneja Miradi wa Airtel Kanda ya Ziwa, Joseph Mushi amesema huduma ya kutuma fedha bila makato ni mkombozi kwa wafanyabiashara wote waliokuwa wakilazimika kupunguza fedha kwa lengo la kukidhi matakwa ya makato.

“Airtel siku zote inakwenda na wakati na mabadiliko ya soko, mfanyabiashara hawezi kupata faida iwapo makato ya kutuma fedha yatakuwa makubwa, hivyo hawatakuwa na uwezo wa kuiunga mkono Serikali inayolenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kata,” amesema Mushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles