25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Nabl: Mji unaongoza kuwa na paka wengi kuliko watu

KAFR NABL, Syria

BAADA ya miezi kadhaa ya mashambulio ya mabomu kutoka kwa vikosi vya Syria na Urusi, mji wa Kafr Nabl,Syria sasa umesalia kuwa makazi ya paka wengi kuliko watu.

Watu wachache waliosalia katika mji huo wa Syria, uliolipuliwa wanajiliwaza na mamia au pengine maelfu wa paka, kama ilivyobaini BBC.

Baadhi ya wakaazi hujificha chini ya kifusi cha nyumba zilizobomolewa ili kujikinga dhidi ya mabomu yanayodondoshwa kutoka angani.

Mmoja wao, ni Salah Jaar mwenye umri wa miaka 32, lakini kama unavyoona hayuko peke yake.

Katika kifusi kilicho karibu naye kuna mamia ya paka waliojipata katoka hali kama yake.

“Unafarijika paka akiwa karibu nawe,” alisema. ‘Zinafanya sahali milipuko ya mabomu, kuporomoka kwa majengo, mateso, na uwoga.”

Nyumbani kwa Salah katika mji wa Kafr Nabl, wakati mmoja ulikuwa makazi ya watu 40,000, sasa ni watu chini ya 100 waliosalia.

Ni vigumu kubaini ni paka wangapi waliopo hapo, ni mamia kwa hakika lakini huenda wamefikia maelfu.

“Watu wengi wamehama mji wa Kafr Nabl hali iliyofanya idadi ya watu kuwa ndogo sana. Kwa kuwa paka wanahitaji watu wakuwatunza kuwapa maji na chakula, wamehamia katika nyumba za watu walioamua kubaki katika mji huo mahame. Kila nyumba ina karibu paka 15, au hata zaidi,” Salah anasema.

Salah bado anafanya kazi ya uandishi habari kituo cha radio cha, Fresh FM, japo studi za kituo hicho zilibomolewa katika mashambulizi ya angani ya hivi karibuni.

Walikuwa na bahati shughuli za kituo hicho zilihamishiwa mji ulio karibu kutokana na sababu za kiusalama,muda mfupi kabla ya mashambulio hayo.

Kituo hicho ambacho huwatangazia watu kuhusu kitisho cha mashambuliuo kupitia habari, na vipindi vingine kilipata umaarufu kutokana na paka.

Makumi kati ya paka hao walifanya ofisi za kituo hicho kuwa makaazi yao. Muasisi wa kituo hicho na mwanaharakati Raed Fares, aliyeuawa na wanamgambo wa Kiislam wenye silaha mwezi Novemba, mwaka jana, alitenga fedha za kuwanunulia maziwa na chakula.

“Paka wengi walizaliwa katika jengo hilo. Mmoja wao aliyekuwa na rangi nyeupe na madoa ya hudhurungi alimpenda sana Raed. Angeliandamana nae kila mahali na hata kulala kando yake,” anasema Salah.

Anapondoka katika mabaki ya iliyokuwa nyumba yake, anakaribishwa na sauti za paka kutoka kila upande, Hili humfanyikia kila mtu, anasema.

Kundi la paka katika barabara za mji wa Kafr Nabl

“Wakati mwingine tunapotembea njiani tunaweza kupatana na paka 20 au 30 wanaoandamana na sisi kila tunapoenda. Baadhi yao walitufuata hadi nyumbani.”

Giza linapoingia milio ya mbwa wasio na wenyewe husikika kutoka kila upande wa mji huo. Wao pia wana njaa na hawana pakwenda. Hali ya kupigania mabaki ya chakula na mahali pa kulala inawafanya kushindana na paka wa Kafr Nabl.

Wengi wao, walikuwa wanapendwa  na familia zilizotoroka mji huo baada ya vikosi vya utawala wa Syria kuanzisha oparesheni ya kuukomboa mji wa Idlib mwezi Aprili iliyopita.

Sasa baada ya kukosa wa kuwatunza na chakula cha mara kwa mara wamelazimika kutafuta makaazi mapya chini ya kifusi cha mijengo iliyoporomoka.

Na japo watu kama Salah hawana matumaini ya kuishi, bila kujua chakula kinatoka wapi, wanajiliwaza na paka hawa ambao wamegeuka kuwa marafiki wa dhati.

“Kila ninapokula, nao hula, iwe ni maboga, spageti au hata mkate uliokauka. Katika hali hii nahisi sote ni viumbe wadhaifu na tunahitaji kusaidiana,” anasema.

Sio ajabu kwa paka kujeruhiwa pamoja na watu kutokana na mashambulio ya mabomu ya mara kwa mara.

Lakini licha ya uhaba wa dawa, sawa na vifa vingine muhimu, Salah anasema wanajaribu kila wanaloweza kuwatunza paka hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles