29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mzee Moyo: Sina mpango kujiunga chama chochote

hassan-nassor-moyoNa Elizabeth Hombo, aliyekuwa Tanga

MWASISI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mapinduzi ya Zanzibar, Nassor Hassan Moyo amesema hafikirii kujiunga na chama chochote cha siasa, baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM.

Wiki iliyopita, Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja, Aziza Iddi Mapuri alitangaza kumfukuza mwanasiasa huyo mkongwe kwa madai ya kukisaliti kwa kukiuka maadili na kutoa matamshi yasiyokubaliana na sera za chama chake.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA nyumbani kwake mkoani Tanga juzi, Moyo alisema umri wake haumruhusu kujiunga na chama chochote cha siasa, lakini ataendelea kuitetea Zanzibar.
“Sina mpango wa kujiunga na chama chochote cha siasa kwa sababu umri wangu hauruhusu, nitaendelea kuungana na wale wote wanaopenda maendeleo ya Zanzibar na wale wanaounga mkono muundo wa serikali tatu, nitashirikiana nao vyovyote iwavyo,”alisema Moyo.
Mzee Moyo aliyepata kushika nyadhifa mbalimbali, alisema tatizo kubwa linaloisumbua CCM ni kwamba hakitaki kukosolewa jambo ambalo wanadhani linawapa nguvu wapinzani.
“CCM wanadhani nchi hii ni yao, kumbe ni ya Tanganyika na Zanzibar. Fikiria kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Warioba, tulipeleka maoni yetu ya kamati ya maridhiano na baadaye tukaiunga mkono, lakini Rais Dk.Ali Mohamed Shein aliwahi kusema haitambui kamati yetu.
“Hatuna shida na Rais Shein, bali tuna shida na wananchi tu na si lingine. Sasa wamenifukuza lakini nitaendelea kutetea maoni ya wananchi,”alisema.
Akizungumzia alivyoshiriki mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema hakuibuka tu, bali alialikwa kama mwenyekiti wa kamati ya maridhiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles