29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti: Watanzania hawataki Serikali kuingilia vyombo vya habari

Elias Msuya, Dar es Salaam
ASILIMIA 65 ya Watanzania wanapenda kuona vyombo vya habari vikichunguza ufisadi unaofanyika serikalini.
Hayo yamo katika ripoti ya Afrobarometer ya mwaka 2014, inayotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo na Kuondoa Umaskini (Repoa).
Ripoti hiyo, imekuja wiki chache baada ya Bunge la Tanzania kupitisha miswada ya Makosa ya Mtandao na Sheria ya Takwimu katika habari za mwaka 2015, zinazokosolewa na wadau, huku wakimshinikiza Rais Jakaya Kikwete asitie saini ili ziwe sheria.
Kwa mujibu wa tovuti ya Repoa, idadi ya Watanzania imeshuka kwa asilimia 15 ukilinganisha na utafiti wa mwaka 2012, huku idadi ya watu wanaoona habari za kukosoa zinahatarisha amani ya nchi ikipanda kutoka asilimia 18 hadi 31, mwaka 2014.
“Theluthi mbili ya Watanzania wanasema vyombo vya habari vinapaswa kuchunguza na kueleza makosa ya Serikali na rushwa na wengi wanasema vyombo hivyo viendelee kuripoti habari na maoni bila kuingiliwa na Serikali.
“Watanzania wameonesha kuridhishwa na umakini wa vyombo vya habari kama wafuatiliaji wa mambo,” imesema ripoti hiyo.
Ripoti hiyo, pia imeonesha asilimia 96 ya Watanzania wanaridhika na uhuru wa kujieleza, huku asilimia 53 wakitaka Serikali kutoingilia kinachochapishwa au kutangazwa na vyombo vya habari.
“Asilimia 76 ya Watanzania wanapendekeza umakini wa vyombo vya habari katika kuchunguza na kuripiti kuhusu rushwa. Hata hivyo idadi hiyo imeshuka kwa asilimia 8 ya mwaka 2012,” imesema ripoti hiyo.
Tanzania inatarajia kuwa na Sheria ya Uhuru wa Habari mwaka huu, baada ya kucheleweshwa mara tano na Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles