Mzee Matata wa Mizengwe afariki dunia

0
392

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Msanii wa Vichekesho aliyejizoelea umaarufu nchini kupitia kipindi cha ucheshi cha Mizengwe, Jumanne Alela maarufu ‘Mzee Matata’ amefariki dunia jana saa 5:30 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alilazwa tangu Juni 13, 2021.

Muigizaji mwenziye wa Tamthilia ya Mizengwe Mkwere Original amesema Mzee Matata alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Kisukari kwa muda mrefu na ndio uliomsababubisha umauti.

Aidha, Mkwere amesema kwa mujibu wa familia ya Mzee Matata, msiba upo Mbagala Chamanzi kwa Mkongo na mazishi yatafanyika kesho saa 7:00 Mchana kwenye makaburi ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here