23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

“Siafiki, tathimini ifanyike ujenzi barabara ya mji wa Serikali”- Prof. Shemdoe

Nteghenjwa Hosseah, Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe ameagiza ifanyike tathmini ya kina ya muda wa nyongeza ulioombwa na Mkandarasi wa barabara za Mji wa Serikali Mtumba zinazojengwa kiwango cha lami.

Mradi huo kwa sasa ujenzi wake umefika asilimia 70 na unatakiwa kukamilika mwezi ujao lakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya China Heinan International Cooperation Co.Ltd (CHICO), ameomba nyongeza ya miezi 10 ili kukamilisha asilimia 30 iliyobaki.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, leo Jumatano Juni 16, 2021, Prof.Shemdoe amesema mradi huo ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi 18 ambapo kwa mujibu wa mkataba ni Julai 31, 2021.

“Kazi imefanyika tumeiona na kiwango kilichofikia ni asilimia 70, gharama ya mradi huu ni Sh bilioni 89.1 na barabara zinazojengwa jumla ni kilometa 51.2 kazi iliyofanyika ni kubwa, tunajua hadi Julai 31, 2021 hii kazi ya asilimia 30 iliyobaki itakuwa bado haijakamilika.

“Mkandarasi kuomba nyongeza ya muda ya miezi 10 hili ombi sijaliafiki nimemuagiza mkandarasi Mshauri wa mradi huu kwamba pamoja na maombi hayo afanye tathmini ya kina ya maombi hayo lakini mimi sijaafiki.

“Hiyo miezi ni mingi iliyoombwa kama mradi huu umetumia miezi 16 kujenga kwa asilimia 70 sioni sababu ya mkandarasi atumie miezi 10 kukamilisha asilimia 30 iliyobaki, namuelekeza Mshauri kwa kushirikiana na TARURA na Meneja wa Mradi wahakikishe wanafanya tathmini ya kina ya muda ulioombwa ili kupata muda muafaka na kazi iishe mapema,”amesema Prof. Shemdoe.

Pia ameagiza kuangalia namna ya kuhusisha suala la upandaji miti kwenye barabara hizo na pia vijengwe vibanda vya abiria kwa ajili ya kusubiri usafiri.

Aidha, amewahakikishia kuwa hati za malipo zote zilizowasilishwa za Sh bilioni 44 kwa mkandarasi zote zimelipwa.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan alihakikisha madeni yote yaliyokuwa yamebaki yamelipwa na tumezilipa na mimi nimesaini malipo yale, mkandrasi asije kulalamika anaidai serikali haidai serikali,” amesema Prof. Shemdoe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles