23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MWILI WA KINARA VITA YA UJANGILI KUAGWA KESHO

Na KAMILI MMBANDO

DAR ES SALAAM

MWILI wa  mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo wa nchi za Afrika, Wayne Lotter, aliyeuawa kwa kupigwa risasi, unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya baobab village Masaki jijini Dar es Salaam.

Lotter ambaye ni raia wa Afrika Kusini alikuwa mkurugenzi na mwanzilishi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Pams Foundation ambayo inajihusisha na kupambana na ujangili wa meno ya tembo barani Afrika.

Inadaiwa mkurugenzi huyo aliuawa kwa kupigwa risasi  usiku wa Agosti 16 akiwa anatoka uwanja wa ndege akielekea nyumbani kwake Masaki na kufariki papo hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya familia jana, Krissie Clark alisema wanatarajia kuaga mwili wa ndugu yao na kupelekwa nyumbani kwao Afrika ya Kusini kwa maziko.

Aidha Krissie alisema kuuawa kwa mwanaharakati huyo hakutawafanya kurudisha nyuma mapambano dhidi ya ujangiili kwani hivi sasa ndio wameelekeza nguvu kubwa katika nchi za Afrika na watahakikisha wanatokomeza kabisa kama ilivyokuwa ndoto ya marehemu Lotter.

Kifo cha mwanaharakati huyo kimeacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu hasa ikizingatiwa kuwa amesaidia kwa kiasi kikubwa kukamatwa kwa vinara wengi wa dawa za kulevya akiwamo malkia wa meno ya tembo.

Akizungumzia kifo hicho mwishoni mwa wiki, waziri wa Maliasili na UItalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema serikali haijafanikiwa kufahamu lengo la watekelezaji wa mauaji hayo.

Inaelezwa kuwa tangu mwaka 2012 aliwezesha jumla ya wawindaji 2,000 wa tembo na wasafirishaji kukamatwa huku akitajwa kusaidia kupunguza mauaji ya wanyama hao kwa karinu asilimia 50

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles