33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE WA SEGEREA ATOA SOMO KWA WAZAZI

Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Segerea, Bonnah Kaluwa (CCM),  amewataka wazazi nchini kujenga mazoea na ushirikiano wa karibu na walimu kwa lengo la kudumisha taaluma na maadili ya watoto wao shuleni, huku akipongeza shule za Tusiime kwa kuwa na ushirikiano mzuri na wazazi

Kaluwa ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam jana wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki katika risala yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Dk. John Mbogoma.

“Ni vyema wazazi mkajitengea muda mzuri wa kutembelea shuleni kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya watoto na inapobidi kutoa ushirikiano wenye tija kwa walimu pale inapohitajika,na hata wakirudi nyumbani wakati wa likizo kazi iwe ile ile hatua ambayo naamini itazidi kuwajenga kitaaluma” alisema Kaluwa

Alisema anapendezwa sana na namna shule hiyo ya Tusiime inavyotoa ushirikiano kwa wazazi pamoja na inavyofanya vyema kitaaluma, jambo linalompa faraja kubwa kutokana na jinsi shule hiyo inavyoiwakilisha vyema Jimbo lake la Segerea analoliongoza.

Awewataka walimu kuzidisha ujuzi na maarifa ili shule hizo ziendelee kufanya vyema katika mitihani mbalimbali ya kikanda na kitaifa ili kulitangaza jimbo la Segerea katika mipaka mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Tusiime Emily Rugambwa aliwapongeza wazazi kutokana na ushirikiano wanaoutoa kwa walimu na uongozi wa shule hiyo, amewataka wahitimu wote kwenda kuwa mabalozi wazuri kipindi watakaporudi mtaani.

Alisema tangu kuanzishwa kwa shule ya sekondari ya Tusiime mwaka 2006 kama sehemu za shule za Tusiime kama muendelezo wa shule za awali na msingi tangia mwaka 1977, wamezidi kuendelea kukua na kupanuka kwa kasi siku hadi siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles