31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

MWENYEKITI HALMASHAURI IGUNGA AKAMATWA KWA AGIZO LA MAJALIWA

Na MURUGWA THOMAS -TABORA


MWENYEKTI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Peter Onesmo na Ofisa Kilimo, Josea Bwenda, wanashikiliwa na polisi kwa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakituhumiwa ubadhirifu wa mradi wa Kijiji cha Choma Chankola.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley, alisema pia watuhumiwa wengine zaidi ya 10 nao wanashikiliwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa mradi wa mashine ya kukoboa mpunga wenye thamani ya Sh milioni 35.

Akitoa taarifa hiyo jana, aliwataja baadhi ya watuhumiwa ni Daudi Mangaluke, Gasper Ulimba, Paul Msafiri, Azizi Kazilo, Yusta Thomas, Jane Kapina, Irene Edward na John Fumbuka.

Alisema baada ya kukamatwa, uchunguzi umefanyika na tayari jalada la kesi hiyo limepelekwa ofisi ya mwanasheria wa Serikali kuwaandalia mashtaka ili wafikishwe mahakamani.

Kukamatwa watuhumiwa hao kunatokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho yaliyotolewa katika mkutano wa hadhara na Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali mbele ya Majaliwa, aliyekuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Tabora hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles