23 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mwanamke wa Thailand atuhumiwa kwa mauaji ya marafiki 12 kwa sumu ya Cyanide

Bangkok, Thailand

Polisi wa Thailand wanasema wamemkamata mwanamke anayeshukiwa kuwaua marafiki zake 12 na jamaa kwa kuwapa sumu ya cyanide

Sararat Rangsiwuthaporn alikamatwa mjini Bangkok siku ya Jumanne kufuatia uchunguzi wa hivi karibuni kuhusu kifo cha rafiki yake.

Familia ya mwathiriwa iliibua tuhuma baada ya kufariki wakiwa safarini na Sararat mapema mwezi huu.

Kufuatia uchunguzi, polisi wiki hii walisema wanaamini kuwa Sararat aliwaua watu wengine 11, akiwemo mpenzi wake wa zamani.

Polisi wanadai aliua kwa sababu za fedha. Sararat amekana mashtaka yote. Mamlaka ya Thailand imemnyima dhamana.

Wiki mbili zilizopita, alikuwa amesafiri na rafiki yake katika jimbo la Ratchaburi, Magharibi mwa Bangkok, ambapo walikuwa wameshiriki katika ibada ya ulinzi wa Wabudha kwenye mto, polisi walisema.

Muda mfupi baadaye, rafiki yake Siriporn Khanwong alianguka na kufa kwenye ukingo wa mto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles