23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanajeshi aliyeuwa watu 26 auawa

Bangkok, Thailand

MWANAJESHI aliyewaua watu 26 kwa bunduki katika mji wa Nakhon Ratchasima, Thai ameuawa kwa kupigwa risasi na maofisa wa usalama, kwa mujinu wa taarifa iliyotolewa na polisi wa Thai.

Jumamosi, Jakraphanth Thomma alimuua kamanda wa polisi na kuiba silaha katika kambi ya jeshi.

Mshukiwa huyo aliendelea kuvamia raia waliokuwa katika shughuli zao barabarani kwenye mji wa kibiashara wa Nakhon Ratchasima, ambao pia unafahamika kama Korat.

Mwanamume huyo ambaye alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wakati anafanya mashambulizi, alipigwa risasi baada ya kuzingirwa usiku kucha katika jengo alilokuwemo.

Waziri Mkuu wa Thailand, Prayuth Chan-ocha, jana alisema kwamba idadi ya waliouawa ni zaidi ya 20 iliyoripotiwa awali na wengine 57 wamejeruhiwa.

“Hiki ni kisa cha kwanza kutokea Thailand, na ninataka hii iwe mara ya mwisho kisa kama hiki kinatokea,” alisema hayo baada ya kutembelea waliojeruhiwa katika hospitali ya Nakhon Ratchasima.

Aliongeza kwamba nia ya shambulio hilo inasemekana ni kulipiza kisasi baada ya mshambuliaji Jakraphanth kuamini kwamba amelaghaiwa katika makubaliano ya kununua kipande cha ardhi.

Taarifa za awali zilisema kuwa mshambuliaji huyo, 32, alijaribu kutoroka kupitia mlango wa nyuma.

Mama yake mshambuliaji pia aliletwa kwenye eneo la tukio ili kumshawishi mtoto wake ajisalimishe.

Mmoja kati ya waliookolewa aliiambia BBC jinsi yeye na wenzake walivyojificha chooni ghorofa ya nne kabla ya kutoroka hadi ghorofa ya pili na kujificha chini ya meza moja mgahawani kwa saa tatu, ambapo walisikia karibu milio minne ya risasi kabla ya kuona wanajeshi waliokuja kuwaokoa.

Charlie Crowson, mwalimu anayefunza Kiingereza ambaye anaishi Nakhon Ratchasima, aliiambia BBC miili ya watu waliokufa imetapakaa barabarani katika mji ambao kawaida huwa na Amani.

Shambulio hilo lilianza karibia saa 9:30 jioni Jumamosi katika kambi ya jeshi ya Suatham Phithak, ambapo kamanda wa polisi Anantharot Krasae aliuawa.

Mkwe wa kamanda huyo mwenye umri wa miaka 63 na mwanajeshi mwengine pia waliuawa. Mshukiwa alichukua silaha kutoka kambini na kuingia kwenye gari.

Kisha alianza kufyatua risasi katika maeneo kadhaa kabla ya kuwasili katika eneo la kibiashara saa 12 jioni siku ya Jumamosi.

Video zilizooneshwa na vyombo vya habari vya eneo vinamuonesha mshukiwa akitoka ndani ya gari na kuanza kufyatua risasi huku watu nao wakikimbilia usalama wao.

Picha kupitia CCTV inamuonesha mshukiwa akiwa ndani ya jengo la kibiashara akiwa ameinua bunduki.

Akiwa anaendelea kushambulia raia, aliandika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii na kuuliza swali, ikiwa ajasilamishe.

Awali alikuwa ametuma picha ya bastola na seti tatu za risasi na kuandika, sasa ni wakati wa kufurahia na hakuna ambaye anaweza kuepuka kifo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles