24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Walioaga dunia kwa Corona China wapindukia 800

BEijing, China

Idadi ya watu waliofariki dunia nchini China kwa ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha corona imepindukia 811 huku maafisa wa afya wa nchi hiyo wakitangaza kuwa, watu 1,439 waliokuwa wameambukizwa kirusi cha corona wamepona.

Kituo cha Afya cha Mkoa wa Hubei kimetangaza kuwa, kufikia juzi, Februari 8 watu 2,147 waliambukizwa kirusi cha corona ambapo 1379 walitoka kiatika mji wa Wuhan huku watuu 81 wakipoteza maisha juzi.

Ripoti iliyotolewa na Kamisheni ya Taifa ya Afya ya China ilieleza jana kuwa kesi mpya 3,399 za watu walioambukizwa kirusi cha corona ziligunduliwa nchini humo na kuifanya idadi ya walioambukizwa ifikie watu 34,546.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, hali za wagonjwa zaidi ya 6000 walioambukizwa virusi vya corona ni mbaya.

Kuzuka kwa kirusi cha corona nchini China kumesababisha nchi kadhaa kuchukua hatua za kupiga marufuku wasafiri wanaotoka China kuingia katika nchi hizo na pia kuwahimiza raia wao kutofanya safari kuelekea China. Baadhi ya nchi zimewashauri hata raia zao walioko China waondoke nchini humo.

Virusi vya Corona viliibuka mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana katika mji wa Wuhan wa Mkoa wa Hubei nchini China, ambapo mbali na kuenea katika mikoa mingine 30 ya nchi hiyo, vimezikumba nchi nyingine za dunia ikiwemo Marekani, Australia, Thailand, Malaysia, Korea Kusini, Japan, Canada, Sweden, Hispania, Ufaransa na Emirates (UAE).

Kwa mujibu wa Reuters, idadi hiyo ya zaidi ya watu 800 waliokufa kwa corona imezidi ya waliokufa kwa SARS mwaka 2003.

Taarifa ya Shirikala Afya Duniani (WHO) iliyotolewa juzi ilieleza kuwa watu waliokufa duniani kote kutokana na ugonjwa wa SARS miaka 17 iliyopitailifikia 774, hivyo ndani ya mwezi mmoja, corona imepitilia idadi hiyo ya vifo.

Taarifa iliyotolewa leo na WHO inasema, hata hivyo, kuna dalili za maambukizi ya kirusi hicho cha corona kuanza kudhibitiwa.

Maambukizi ya kirusi cha SARS katika mwaka 2002 hadi 2003 yaliuawa watu 774 duniani kote.

Takwimu za hivi karibuni kabisa za WHO zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizo kimepunguwa kwenye mji wa Hubei, ambao ndio kitovu cha kirusi cha corona, lakini imeonya kuwa bado idadi ya wanaopoteza maisha inaweza kuongezeka.

Hayo yanajiri wakati idara ya Hong Kong ikitangaza kuwa abiria wote 3,600 pamoja na wafanyakazi waliokuwa wamewekwa karantini katika meli ya anasa ya World Dream, wataruhusiwa kuondoka.

Kulingana na idara hiyo, vipimo vilivyochukuliwa kutoka abiria 1,800 vimeonesha kuwa abiria hao hawajaambukizwa virusi vya corona.

Meli hiyo ilikuwa imezuiliwa mjini Hong Kong siku ya Jumatano wiki iliyomalizika,  baada ya maofisa wa China Bara kuwajulisha wafanyakazi wa meli hiyo kuwa abiria wao watatu wameambukizwa virusi hivyo. Hadi sasa, watu zaidi ya 37,500 duniani wameshaambukizwa virusi hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles