28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAHABARI ALIYEKIMBILIA FINLAND AJA KIVINGINE



Na MWANDISHI WETU

MWANDISHI wa habari ambaye alikimbilia nchini Finland  kwa madai ya kuwakimbia aliowaita ‘wauaji’ wake, Ansbert Ngurumo amekuja kivingine kwa kutoa wimbo wenye jina ‘Naililia Tanzania’.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Ngurumo alisema aliamua kutunga wimbo huo kwa kuwa nchi inapitia katika kipindi kigumu kisiasa, kiuchumi, kijamii hata kiimani.

“Haya si mambo ya kuchekelea, wengi wanaumia, wanalia hivyo nalia pamoja nao lakini haitoshi kulia. Kama raia huru, tunawajibika kutetea taifa letu ili lisianguke zaidi.

“Vilio visiongezeke, taifa lirejee kwenye misingi yake, amani na usalama vipatikane na ustawi wa kitaifa upatikane.

“Ili hayo yawezekane, ili tupate nguvu ya kupambana na madhila hayo, sharti kwanza tuwe hai, tuwe na afya njema. Hayo hayapatikani kwingine isipokuwa kwa Mungu. Ndiyo maana lazima pia tumwombe Mungu mwenye Huruma asikilize kilio chetu na asimame nasi tunapopambana na dhuluma na ukatili huu,”alisema.

Akifafanunua kuhusu wimbo huo, alisema una beti 18 na kibwagizo cha mistari saba na sehemu ya tatu.

Ngurumo ambaye pia ni mwanasiasa, alisema sehemu ya kwanza una ujumbe wa jumla juu ya hali halisi ya Tanzania ilivyo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

“Sehemu ya pili; ala kama kiungo na kiburudisho kati ya tenzi na tenzi. Ni muziki unaochezeka na kuimbika kirahisi, sehemu ya tatu; kibwagizo cha mwisho kama hamasisho la umma.

“Ni muziki unaomhusu kila raia wa Tanzania. Ni muziki wa kizalendo unaopiga vita ufisadi, ukatili, ubaguzi, wizi na matumizi mabaya ya madaraka. Unahamasisha amani, haki, umoja, na usalama. “Unagusa wanasiasa, viongozi wa dini, wafanyabiashara, wanaharakati, wanataaluma na wananchi wote kwa ujumla,”alisema Ngurumo.

Alisema utazinduliwa wakati wowote ndani mwezi ya huu kwa utaratibu maalumu utakaotangazwa.

Machi Mwaka huu, Ngurumo alikimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi ya muda baada ya kudai kuwa ametishiwa kifo na watu wasiojulikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles