27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA KITILA AONYA MIGOGORO SEKTA YA MAJI

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, amewataka wanasheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na taasisi zake kuhakikisha wanasimamia sheria wanazoziweka, ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kuisababishia Serikali hasara na kukwamisha maendeleo ya Sekta ya Maji.

Profesa Mkumbo aliyasema hayo jana katika mkutano uliowakutanisha wanasheria 36 kati ya 41 kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, pamoja na wanasheria wa wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma, wenye lengo la kuboresha utendaji wa wanasheria katika Sekta ya Maji katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango.

Alisema kama washauri na wasimamizi wa sheria katika Sekta ya Maji, waendelee kusimamia vyema sheria, taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali na kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na ufanisi.

‘‘Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika sekta yetu, mmekuwa mkitatua migogoro mingi ya kisheria na kuisaidia Serikali katika mambo mengi ya msingi.

‘‘Jambo la msingi ni kuhakikisha mnasimamia misingi ya sheria mnazoziweka ili kuisaidia Serikali kuepukana na hasara na migogoro ambayo itakwamisha maendeleo ya Sekta ya Maji, huku mkifanya kazi yenu kwa weledi na uadilifu,’’ alisema Profesa Mkumbo.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Simon Nkanyemka, alisema watatumia mkutano huo kufahamiana, kujifunza, kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili changamoto wanazokumbana nazo na mbinu za kuzitatua

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles