23.4 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi China aliyekula ‘wali na pilipili’ kwa miaka mitano kumuuguza ndugu yake afariki

GUIZHOU, CHINA

MWANAFUNZI nchini China ambaye alikuwa akila wali na pilipili kwa miaka mitano ili aweze kuweka akiba ya kumwezesha kumtunza ndugu yake mgonjwa amefariki, vyombo vya habari vya China vimeeleza.

Hali ngumu iliyokuwa ikimkabili Wu Huayan ambaye alikuwa amefikisha kilo 20 iliishtua Serikali ya China mwaka jana na kuzua mijadala mikali.

Oktoba 2019 alilazwa hospitalini  baada ya kupata tatizo la kupumua.

Michango ilifurika kwa ajili ya kumsaidia kurudi katika afya njema, lakini kaka yake aliwaambia wana habari kuwa alifariki siku ya Jumatatu.

Wu aliliambia gazeti la Chongqing kuwa alivigeukia vyombo vya habari ili kuomba msaada baada ya kushuhudia baba na bibi yake wakifariki kwa kuwa hawakuwa na fedha za kulipa matibabu.

”Sitaki kushuhudia hayo tena -kusubiri kifo kwa sababu ya umasikini,” alisema.

Kaka yake, ambaye hakutajwa jina lake, aliliambia gazeti la vijana la Beijing kuwa ndugu yake huyo amefariki akiwa na miaka 24.

Mwaka jana, madaktari walisema mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu alikuwa na maradhi ya moyo na figo kutokana na miaka mitano aliyokuwa akila chakula kidogo sana.

MAISHA YAO

Wu Huayan na kaka yake waliishi katika mazingira magumu kwa miaka mingi baada ya kufiwa na wazazi wao wakiwa wadogo.

Yeye na ndugu yake walilelewa na nyanya na baadaye mjomba na shangazi ambao waliweza kuwapatia Yeni 300 (sawa na shilingi za kitanzania 100,376) kila mwezi.

Sehemu kubwa ya fedha hizo zilitumika kulipa matibabu ya ndugu yake mdogo ambaye alikuwa anakabiliwa na changamoto za kifua.

Hii ilimaanisha Wu alitumia yeni mbili (sawa na Shilingi 669) kwa siku ambayo ilimwezesha kununua mchele na pili pili kwa miaka mitano.

Alipowasili hospitali alikuwa na na urefu wa futi nne na nusu (4ft 5in).

Madaktari walisema alikuwa katika hali mbaya kutokana na ukosefu wa lishe kiasi cha kupoteza asilimia 50 ya nywele zake kichwani.

Ndugu hao ambao wanatokea mkoa wa Guizhou, moja ya mikoa masikini zaidi nchini China na kisa hiki kimetoa taswira ya hali mbaya ya umasikini nchini China.

Japo uchumi wa China umekuwa kwa miongo kadhaa iliyopita viwango vya umasikini havijapungua, huku takwimu ya kitaifa ya mwaka 2017 zikionesha kuwa takribani watu milioni 30.46 wanaoishi katika maeneo ya mashambani wanaishi chini ya dola 1.90 kwa siku.

Viwango vya ukosefu wa usawa pia viliongezeka huku ripoti ya mwaka 2018 ya shirika la fedha duniani,IMF, likisema kuwa China ni ”moja ya mataifa yasiyokuwa na usawa duniani”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles