25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

Mwalimu Mkuu atuhumiwa kumpa ujauzito mwanafuzi wake

Na Upendo Mosha, Hai

Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Sawe iliyopo katika Kijiji cha Sawe Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, Solomoni Sirikwa anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Mei 23, 2019 wilayani humo Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Emmanuel Mushi, amesema jumla ya wanafunzi watatu wamepewa ujauzito mwaka huu wa masomo 2019 na mmoja wao anatuhumiwa kupewa ujauzito na Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo.

Mushi amesema wanafunzi waliopewa ujauzito mwaka huu wa masomo wapo watatu, kidato cha nne, kidato cha tatu na kidato cha pili na watuhumiwa note wamekimbia hawajulikani walipo.

“Hadi sasa tunapozungumza wanafunzi hao wamesimamishwa shule na uongozi wasiendele na masomo baada ya kupimwa na kubainika kuwa wajawazito” amesema Mwenyekiti huyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Secilia Kullaya, amekiri kuwepo kwa wanafunzi hao waliopata ujauzito na suala hilo limeripotiwa katika vyombo vya usalama ili watuhumiwa waliohusika watafutwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Taarifa za uhalifu huu tumeshazifikisha katika vyombo vya dola hivyo tunasubiri wahusika watafutwe na kukamatwa ili sheria ifuate mkondo wake,” amesema Mwalimu Secilia.

Aidha Mwenyekiti wa Kijiji kingine cha Chekimaji Kata ya Masama Rundugai, Selemani Juma, amesema katika Shule ya Msingi ya Chekereni iliyopo katika kijiji chake mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka (12) naye amekutwa ana ujauzito.

Mwenyekiti huyo amedai kupata taarifa hizo kutoka kwa wananchi na alipofuatilia kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo alikiri kuwepo kwa mwanafunzi huyo.

“Baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa mwanafunzi wa darasa la saba mwenye ujauzito katika kijiji changu nikachukua jukumu la kumuuliza Mwalimu Mkuu wa Shule anayosoma binti huyo na kukubali kuwa taarifa hizo ni za ukweli,” amesema Selemani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,089FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles