23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kesi ya mfanyabiashara aliyejeruhi yaahirishwa hadi Juni

JANETH MUSHI -ARUSHA

Kesi ya kujeruhi watu wawili kwa kuwakata masikio inayomkabili mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha, Anselim Minja, imeahirishwa hadi Juni 21 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokukamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arumeru, Amalia Mushi ,Minja anadaiwa kuwakata masikio ya kushoto Samwel Sembeke na Aloyce Petro, ambao kwa sasa wanadaiwa kupata ulemavu wa kudumu.

Wakili wa Jamhuri Ahmed Khatibu, aliieleza Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo upo katika hatua za mwisho na kuiomba Mahakama iiahirishe.

Hakimu Amalia aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 21 mwaka huu ambapo Minja alikuwa akitetewa na Wakili Innocent Mwanga, ambaye hakuwa na pingamizi na maelezo hayo ya Wakili wa Jamhuri.

Minja ambaye anamiliki biashara mbalimbali jijini hapa ikiwemo pamoja na shule ya kujifunzia udereva wa magari(Modern Driving School), kwa mara ya kwanza alifikishwa kizimbani Machi 28 mwaka huu.

Awali mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Obadia Bwegego, akimsomea mashitaka hayo Wakili Mwandamizi wa Serikali, Martenus Marandu, alidai mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo Julai 21 mwaka 2017, katika eneo la Njiro jijini hapa.

Alidai mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo huku akijua ni kinyume cha sheria, ambapo alidai kuwasababishia watu hao ulemavu wa kudumu baada ya kitendo hicho cha kikatili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles