28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu adaiwa kubaka mwanafunzi wa darasa la 7

Shomari Binda -Musoma

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara, linamshikilia Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Bwai A,Wilaya ya Musoma, Lazaro Mmanga kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, akiwa anajiandaa kufanya mtihani wa taifa.

Mwalimu huyo anadaiwa kutenda tukio hilo septemba 4, mwaka huu  kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 ambaye jina lake linahifadhiwa.

Mwalimu huyo, akimfundisha na wenzake somo la hesabu kwa ajili ya kujiandaa mitihani ya mwisho ya elimu ya msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alisema amesikitishwa na tukio hilo na kutaka hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya mwalimu huyo.

Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya walimu kutozingatia maadili na kuingia tamaa ya mwili na kuwaingilia wanafunzi wanaowafundisha jambo ambalo halikubaliki na  kuona mwalimu akikatisha ndoto za mwanafunzi.

Alisema mkoa hauwezi kukubali kuona matukio ya namna hiyo yakiendelea kutokea kwa wachache ambao hawazingatii maadili yao ya kazi na kulitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili mhusika afikishea kwenye vyombo vya sheria.

“Hii ni aibu kubwa aliyofanya mwalimu kumbaka mwanafunzi wake, akiwa anamuandaa na mitihani ya mwisho ya darasa la saba, tunataka tabia hii ikome hatuwezi kukubali wanafunzi na watoto wetu wahalibiwe maisha”,alisema Malima.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki, alisema mwalimun huyo alimpitisha mwanafunzi  dirishani na kumuingiza ofisi ya mwalimu mkuu, kisha kufunga mlango wa kutokea nje na yeye kuzunguka dirishani, kisha kuingia ndani ya ofisi hiyo.

Alisema baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakimwagilia maua pembeni waliona tukio hilo,kisha kutoa taarifa kwa viongozi wa kijiji na kumkamata mwalimu akiwa na mwanafunzi ofisini, kisha kumfikisha kituo cha polisi Mugango.

Kamanda Ndaki alisema baada ya kufikishwa kituoni, baadhi ya wananchi walivamia kituo hicho kwa lengo la kutaka kumuua na kutokea fujo zilizosababisha gari la polisi kupondwa mawe na kutaka kuchomwa moto, polisi walifanya jitihada za kukabiliana na vurugu hizo.

Alisema kutokana na vurugu hizo, watu 42 wanashikiliwa na polisi kutokana uharibifu wa mali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles