Menejimenti TACAIDS yapongezwa

0
623

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamisheni wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Hedwiga Swai ameipongeza menejimenti ya tume hiyo kwa kutekelezaji majukumu yake vizuri hatua ambayo imesababisha kupungua kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kutoka asilimia  5.3 mwaka 2011/12 hadi asiliami  4.7 mwaka 2016/17.

Dk. Swai aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam wakati akihitimisha kikao cha kamisheni ya wajumbe 11 ilipokuwa inaagana na menejimenti ya TACAIDS baada ya kumaliza muda wake wa miakami tatu.

Aliitaka menejimenti kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na juhudi, hasa ikizingatiwa taifa linawategemea kutoa dira ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo.

‘Tunawapongeza,tunawashukuru kwa ushirikiano mzuri mliotupatia toka tulipoteuliwa tunawaomba muendelee kujituma na kutekeleza malengo, mkiendelea kushirikia na bega kwa bega na wadau wetua mbao wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na tumehii,” alisema Dk.Swai.

Aliiagiza menejimenti kutokata tamaa ya kutafuta raslimali fedha za kutekeleza  hatua mbalimbali za mwitikio wa Ukimwi nchini hilo, ni jukumu la tume, kazi mlioifanya ni kubwa laki ni bado jukumu lililopo mbele ye tu ni kubwa zaidi, mjitahidi ifikapo 2030 kuwe hakuna maambukizi mapyatena.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Jumanne Issango aliipongeza  kamisheni  kwa maelekezo mazuri waliyoyatoa kwao.

Wajumbe waliomaliza muda wao ni pamoja na Paulina Mkonongo, Supya Nalengigwa,Naima Mketo,TheophildaKapinga, Sheikh Alhaj Salum, Dk Rosemary Mwaipopo,, Peter Maduki, Derick Mtavangu Mariam Mmbaga na Dk.Leonard Subi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here