24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

MWAKINYO APEWA USHAURI KUPANDISHA KIWANGO

Winfrida Mtoi -Dar es salaam

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mfaume Mfaume, amempa ushauri, Hassan Mwakinyo kukubali kucheza pambano la ngumu ili aweze kupanda baada ya kushuka katika viwango vya Dunia.

Mfaume anayecheza uzito wa kati, ameendelea kushikiria rekodi yake ya namba moja Tanzania na katika viwango vya Dunia vilivyolewa hivi karibuni amepanda kutoka nafasi ya 400 hadi 311 kati ya 1588.

Kwa upande wa Mwakinyo anayechezea uzito wa welter, alikuwa Mtanzania pekee mwenye rekodi nzuri kidunia, lakini katika viwango vilivyotolewa mwezi uliopita ameshika kutoka nafasi ya 18 hadi 78 kati ya 1908.

Akizungumza na MTANZANIA jana,  Mfaume, alisema mara nyingi amekuwa akimtaka bondia huyo kucheza pambano na mabondia wenye rekodi nzuri, lakini amekuwa akikimbilia kupigana na wale wa nje.

Mfaume alisema kwa sababu mabondia aliocheza nao hawakuwa na rekodi nzuri, imefanya yeye kushuka na  kuwapandisha  wenzake.

Alisema baada ya Mwakinyo kubebwa na pambano la Uingereza, kuanzia hapo alitakiwa kucheza na watu walio juu zaidi ili kujiongezea pointi, lakini imekuwa tofauti.

“Mimi nilikuwa nataka kupigana na Mwakinyo, sio kwa kutafuta jina bali nilijua akicheza na mimi atapanda au Watanzania wengine atapanda zaidi,  amekimbilia watu wa nje na matokeo yake ni hayo.

“Mechi alizocheza tangu ametoka Uingereza, ni nyepesi,mfano ile aliyocheza Kenya, nyingine alimpiga Mfilipino hapa nyumbani lakini matokeo yake Mfilipino kapanda Mwakinyo kashuka,” alisema Mfaume.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles