25.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Muziki wa Afrika kuchezwa Marekani leo

AntiqueZIARA ya muziki ya mwimbaji wa Afro Pop kutoka Marekani, Wicks Davis ‘Antique’ nchini Marekani inatarajiwa kuonyesha ubora na vionjo vya muziki wa Afrika aliouandaa baada ya ziara yake ya kimataifa za kimuziki katika nchi hizo.

“Katika ziara yangu hiyo ya ‘The Remember Tour’ nitakuwa nikipiga muziki nilioutengeneza kutokana na ubora na vionjo vya muziki wa Afrika,’’ alisema Antique, alipozungumza na Mtanzania akitokea Marekani.

Onyesho la kwanza linafanyika leo katika ukumbi wa makumbusho Off the Grid, mjini Oakland na onyesho la pili atalifanya katika katika tamasha la ‘Life is Living’, litakalofanyika Oktoba 10 ambalo litajumuisha wasanii maalumu.

Onyesho la tatu na la mwisho katika ziara hiyo litafanyika katika mgahawa mkubwa wa Wajamaica uliopo Kingston 11,  Oktoba 15.

Aliongeza kwamba, muziki wote atafanya ‘live’ akiwa na bendi yake ya wanamuziki saba wa Marekani, ingawa kutakuwa na usaidizi kutoka kwa mpiga gitaa kutoka Senegal.

Antique aliongeza kwamba muziki aliopanga kucheza katika ziara yake hizo unatokana na mchanganyiko wa muziki alioupata katika ziara yake ya kimuziki katika matamasha mbalimbali nchi za Magharibi, ikiwemo Ghana na Mali na Zanzibar kwa Afrika Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles