Kylie Jenner, Tyga kuachana kisa jina la Drake?

0
763

Kylie Jenner, TygaNEW YORK, Marekani

BAADA ya wiki kadhaa za furaha ya nyota wa muziki nchini Marekani, Tyga kumnunulia mpenzi wake, Kylie Jenner, gari aina ya Mercedes G Wagon alipofanya sherehe ya kukumbuka siku ya kuzaliwa kwake, hali imebadilika na kuwa ya huzuni.

Uhusiano wa wawili hao unaonekana kuingiwa na mdudu mbaya baada ya kutokea malumbano kati yao ambapo kwa mujibu wa mtandao wa Hollywood life, chanzo ni kwamba Tyga alimtukana mpenzi wake huyo kwa kumfananisha mambo mabaya na Drake.

Mtandao huo unaeleza kwamba Kylie alimhoji Tyga kwamba, hataki kusikia mashabiki wakiimba baadhi ya nyimbo zake anapokuwa baa kama anavyoimbiwa Drake, ndipo sintofahamu ikaanzia hapo, Tyga akaona amefedheheshwa.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here