25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Muuaji alipanga mashambulizi makubwa

Micah Johnson
Micah Johnson

DALLAS, PAKISTAN

MAAFISA nchini Marekani wamesema Micah Johnson, aliyewashambulia maafisa wa polisi mjini Dallas wiki iliyopita na kuwaua askari watano alikuwa anapanga mashambulizi makubwa zaidi.

Johnson aliwapiga risasi askari 11 katika maandamano ya umma ya kupinga mauaji ya Wamarekani wawili weusi yaliyofanywa na askari weupe.

Mkuu wa Polisi wa Dallas, David Brown amesema uchunguzi katika nyumba ya mshambuliaji huyo ambaye alikuwa mwanajeshi wa Marekani, ulionyesha alifanya majaribio ya kutumia milipuko.

Hayo yanakuja huku maandamano zaidi ya kupinga mauaji ya watu weusi yakishuhudiwa hapo jana kwa siku ya nne mfululizo katika miji kadhaa nchini humo.

Maafisa wa polisi wamewakamata waandamanaji 160 katika mji wa Louisiana waliokwamisha shughuli katika barabara kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles