28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mwana wa Osama kumlipizia kisasi baba yake

hamza-bin-laden
hamza-bin-laden

KARACHI, PAKISTAN

MTOTO wa aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda, Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya baba yake.

Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika mitandao, Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa Marekani kwa kumuua baba yake mwaka 2011 nchini hapa.

Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa kisemacho ‘Sote tu Osama,”Hamza ambaye inaaminika alikuwa na baba yake wakati makomando wa Marekani walipowavamia na kumuua ameapa kuendeleza kazi aliyoianza baba yake.

“Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mmejificha kwa maovu mnayoyaendeleza nchini Palestina, Afghanistan, Syria, Irak, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya Waislamu mnayokalia,” Shirika la Habari la Reuters linamnukuu.

“Na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osama ole wenu, kwa vile sisi tutakuwa tukilinda dini ya Kiislamu,” alisema Hamza.

Hamza ambaye kwa sasa ana umri wa kati ya miaka 20 alikuwa na baba yake kabla ya mashambulizi ya kigaidi ya mwaka wa 9/2001 huko Afghanistan kabla ya kukimbilia Pakistan kufuatia mashambulizi makali ya Marekani na washirika wake.

Hamza kwa mujibu ya wachambuzi anatambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi hilo Ayman al-Zawahiri na ujumbe wake huo unalenga kuwavutia vijana wengi ambao kwa sasa wamejiunga kwa wingi na kundi lijiitalo Dola la Kiislamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles