26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mume na mkewe jela miaka 5 kwa kukeketa watoto

Mohamed Hamad- Simanjiro

MAHAKAMA ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela, Thadei Parokwa (43) na mke wake, Lowema Thadei (34) kwa kosa la kuwakeketa watoto wao watatu.

Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Hamilton Moses, alidai Parokwa na Lowema ambaye ni mama wa kambo wa watoto hao, wanakabiliwa na shtaka ukatili dhidi ya watoto.

Alidai kesi hiyo, iliripotiwa kituo cha Polisi Orkesmet Machi 19, mwaka jana.

Watuhumiwa wanadaiwa kuwakeketa watoto hao kwa bibi yao aliyekuwa anaishi Kitongoji cha Kangala, Kijiji cha Lobosireti.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Lugano Kasebele, baada ya kujiridhisha na ushahidi wa pande mbili, aliwatia hatiani wazazi na kuwahukumu kwenda jela miaka mitano na kulipa faini ya Sh 600,000.

Alisema vitendo vya ukeketaji vimekuwa vikifanyika kwa kificho wilayani humo pamoja na uwepo wa sheria.

Kwa upande wake, Moses, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa wahusika kwani vitendo hivyo vimekithiri wilayani.

“Mheshimiwa hakimu vitendo hivi vimekithiri hapa wilayani Kwetu, naomba utoe adhabu kali kwa wahusika ili iwe fundisho kwa wengine kwani vina madhara makubwa kwa jamii,” alisema Moses.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles