23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

MUME NA MKE WASUSIWA KUCHIMBA KABURI LA MTOTO WAO

NA AMON MTEGA, SONGEA

WAKAZI wa Mtaa wa Namanyigu, Kata ya Mshangano, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma juzi waliwasusia wana ndoa  wawili kuchimba kaburi la kumzikia mtoto wao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wanandoa hao walisusiwa kuchimba kaburi la mtoto wao aliyetajwa kwa jina la Danroad Mahundi (36) kwa madai kuwa kifo chake kilisababishwa na wazazi wake.

Mashuhudu hao ambao hawakutaka majina yao kutajwa, wakazi wa eneo hilo wanawatuhumu wana ndoa kujihusisha na vitendo vya kishirikina, hivyo baada ya kususia uchimbaji wa kaburi shughuli za mazishi hazikufanyika.

Kabla ya tukio hilo, mazishi ya marehemu yalipangwa kufanyika juzi, majira ya saa 6.00 mchana lakini kabla ya kuanza kwa taratibu za mazishi, vijana waliokuwa msibani walisusa kujihusisha na shughuli yoyote kwa madai kuwa wazazi wa marehemu wamesababisha kifo cha mtoto wao hivyo wakachimbe kaburi wao wenyewe.

Walisema wazazi wa marehemu ambao majina yao tumeyahifadhi walikubali sharti la vijana hao la kwenda kuchimba kaburi na walipolikamilisha waligoma kuubeba mwili kwenda kuuzika kwa madai kuwa kuna dalili marehemu hajafa.

Mgomo huo uliibua vurugu ambazo ziliwalazimu kufika eneo la tukio kurejesha hali ya mani kabla ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospital ya Mkoa Ruvuma.

Aidha polisi waliwachukua wana ndoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa tuhuma walizoelekezewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji jana alilithibitishia MTANZANIA kutokea tukio hilo na kueleza kuwa wanandoa hao wanaendelea kushikiliwa hadi uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles