30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

MNH YAFANIKISHA OPARESHENI YA KUSHUSHA KOKWA

Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary

Na VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

MADAKTARI Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamefanikisha upasuaji wa kwanza wa kushusha kokwa za korodani za mtoto mwenye umri wa miaka nane ambazo hazikushuka kama inavyotakiwa.

Upasuaji huo umefanywa kwa kutumia njia ya matundu madogo (Laparoscopic surgery) kwa ushirikiano wa madaktari wa MNH na wa Hospitali ya King Faisal ya Saudi Arabia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Zaituni Bokhary alisema upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa.

“Mtoto huyu mwishoni mwa mwaka jana tulimfanyia upasuaji wa awali wa kuzisogeza karibu kokwa zake kwa sababu zilikuwa ndani mno tumboni, leo (jana) tumemalizia upasuaji kwa kuzishusha rasmi kwenye korodani zake,” alisema.

Daktari huyo alisema kokwa za kiume zinapaswa kushuka na kukaa katika vifuko vya korodani na kwamba iwapo zitaendelea kubakia tumboni husababisha tatizo la kushindwa kutungisha mimba.

Alisema pamoja na mtoto huyo, pia wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji kwa watoto wengine waliokuwa na matatizo mbalimbali.

“Tulianza upasuaji Februari 20, mwaka huu, tumewafanyia watoto sita kati yao wawili walikuwa na tatizo la kokwa zao kutoshuka kwenye korodani, wapo wawili ambao tumewatengeneza njia ya haja kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles